Na Mwandishi Wetu
Jeshi polisi Zanzibar limesema limejipanga kikamilifu kukabiliana na vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa Amani katika kipindi chote cha sikukuu ya pasaka.
Afisa habari Mkuu wa jeshi hilo Inspekta, Mohamed Mhina amesema wameshawaagiza makamanda wa mikoa ya Unguja na Pemba kuimarisha Ulinzi na Usalama katika maeneo ya ibada ya waumini wa Kikiristo.
Amesema jeshi hilo limelazimika kutoa agizo hilo ili kuhakikisha maeneo yote yatakayotumika kwenye mkesha wa ibada hiyo yanafanyiwa doria pamoja na sehemu zote mijini na vijijini ili waumini wa dini ya ili kuepusha uvunjifu wa amani .
Inspekta Mhina amewaomba wananchi kutoa ushirikiano na kutoa taarifa mara watakapobaini dalili za uvunjaji wa sheria au kupanga uhalifu katika maeneo yao.
Ametoa taarifa hiyo vyombo vya habari kwa niaba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame katika kuelekea sikukuu ya pasaka.