Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mufti Mkuu Z’bar asikitishwa na matusi bunge la katiba

$
0
0
Na Mwandishi wetu
WAJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, wametakiwa kuzingatia kile kilichowapeleka Dodoma badala ya kuendeleza lugha za kejeli na matusi.

Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi, alielezea wasiwasi wake juu ya lugha za matusi zinazotumika katika mjadala huo ambao kwa kiasi kikubwa ni kinyume cha maadili ya dini zote ambazo zinahimiza kuheshimiana na kutodharauliana.

Mufti Kaabi alikemea tabia iliyojitokeza katika bunge hiloambapo wabunge wamekuwa wakitukanana matusi ya nguoni na kusahau kwamba Watanzania wanachotegemea kutoka kwao ni michango ambayo itaboresha rasimu hiyo ya katiba iliyo mbele yao.

Alisema kwamba Watanzania wanachotegemea kutoka kwa wajumbe hao ni hoja za msingi katika kutetea misimamo yaona sio kutukanana na kukejeliana.

Aliwataka wajumbe hao wavumiliane pale ambapo mjumbe atasikia hoja ambazo hazitamridhisha na ajiandae kujibu hoja hizo kwa dalili zenye mishiko.


Mufti Kaabi alikitakia kheri kikao hicho ili kifikie makubaliano juu ya katiba muwafaka inayotarajiwa na Watanzania wote.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles