Mwenyekiti wa Baraza la Maichezo Zanzibar BMZ Bi Sherry Khamis, akizindua Bonaza la Ziro Tatu kwa Vijana Kupiga Vita Maambukizo ya Ukimwi Zanzibar,akirusha mpira kulizindua kwa mpira wa peti, Bonaza hilo limeandaliwa na Jumuiya ya ZAYADESA, katika viwanja vya amani nje.
Mratibu wa miradi wa ZAYEDESA nDG. Mgoli Lucian akielezea madhumuni ya Bonaza hilo la Ziro Tatu , na kutoa maana ya ZIRO TATU, ziro ya kwanza ni Kuondoa Unyanyapaa, Ziro ya Pili Kupunguza Vifo kwa Maambukizo ya Ukimwi na Ziro ya Tatu kupunguza na kuondoa Maambukizo kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto Zanzibar. Bonaza hilo limefanyika viwanja vya nje uwanja wa Amani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi. Sherry Khamis, akitowa nasaha zake kwa Vijana wanamichezo walioshirika Bonaza hilo, na kushirikisha michezombalimbali ya Vijana kuhamasisha kuondoa maanbukizo ya Ukimwi kwa Vijana wa Zanzibar.
Katibu wa Jumuiya ya ZAYEDESA Bi. Lucis Majaliwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bonaza hilo lililozinduliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar, katika viwanja vya nje Amani Zanzibar, jumla ya Vijana 400, wameshiriki katika Bonaza hilo.
Washiriki wa Bonaza hilo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar akitowa nasaha zake.Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi. Shery Khamis akiwasalimia baadhi ya Wanamichezi walioshiriki Bonaza hilo baada ya kulizinduwa katika viwanja vya Amani Zanzibar.
Mratibu wa Miradi wa ZAYEDESA Ndg. Mgoli Lucian, akiongozana Wafanyakazi wa ZAYEDESA, kuwasalimia wanamichezo walioshiriki Bonaza hilo la Ziro Tatu.katika viwanja vya Amani.
Washiriki wa Bonaza la Ziro Tatu, wakishiriki mchezo wa netiboli kati ya timu ya Amani na Mpendae, Mchezaji wa timu ya Mpendae akiwa na mpira huku mchezaji wa timu ya Amani, timu Mpendae imeshinda 15--9