Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Hadithi ya leo (12)

$
0
0

 

Mtume Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:

{عليكم بقيام الليل فإنه دأب الصالحين قبلكم، وقربة إلى الله تعالى، ومكفرة للسيئات، ومنهاة عن الإثم [رواه أحمد والترمذي وصححه الألباني].

‘Ni wajibu kwenu kuuhuisha usiku kwa kusali kwani ( kufanya hivyo) ni kuwaiga waliokuwa bora kabla yenu na kuwakurubisha kwa Allaah Subhaanahu Wata’ala, na kuyatolea kafara (kusamehewa) madhambi na kuwakataza na maasi na madhambi’

Imepokewa na  Ahmad na Attirmidhiy na Sheikh Albaani amesema ni sahihi.

Sala za usiku mkubwa (Tahajjud) zina fadhila nyingi na ambazo tukizikosa kwa kutokutumia fursa hii adhimu na nadra ya kuzifanya ibada hizi basi tutakuwa ni wenye kujutia katika maisha yetu.

Mtume wetu Swalla Allaahu ‘Alayhi wasallam aliamrishwa na Mola wake kuamka usiku na kusali na kupangiwa muda iwe nusu ya usiku au thuluthi ya usiku au azidishe kidogo akisoma Qur’aan. ( Suuratu Muzammil 1-4)

Mtume wetu ametuamrisha nasi tuzisali sala hizi kwa kujua umuhimu na fadhila zilizomo ndani yake wakati Mola wetu hushuka hadi mbingu ya duniani na kuwatafuta wenye kumuomba, wenye kufanya ibada, wenye kutaka msaada na kuwatakabalia maombi yao, ibada zao na shida zao zote.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles