Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Balozi Seif: MwanaCCM anaekwenda kinyume na katiba na miongozo ya chama hana sifa za kuitwa mwanaCCM

$
0
0
 Wajumbe wa Halmashauri ya CCM  wa Wilaya za Dimani, Mfenesini na Mkoa wa Magharibi Kichama wakimsikiliza Mlezi wa Mkoa huo Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akikaribishwa rasmi kuwa mlezi wa Mkoa huo katika Mkutano uliofanyika katika Tawi la CCM Kiembe Samaki
 Wajumbe wa Halmashauri ya CCM  wa Wilaya za Dimani, Mfenesini na Mkoa wa Magharibi Kichama wakimsikiliza Mlezi wa Mkoa huo Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akikaribishwa rasmi kuwa mlezi wa Mkoa huo katika Mkutano uliofanyika katika Tawi la CCM Kiembe Samaki
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri ya CCM wa Wilaya za Dimani, Mfenesini na Mkoa wa Magharibi Kichama katika mkutano maalum wa kukaribishwa kwake kuwa Mlezi wa Mkoa Magharibi Kichama.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ
Balozi Seif akikabidhi mchango wa shilingi Milioni 1,000,000/- kununulia Mabati kwa ajili ya uwezekaji wa Tawi la CCM la Kilima Matange liliopo Jimbo la Muyuni kutekeleza ahadi aliyoitoa Mwezi Machi mwaka huu wakati wa ziara yake Mkoa Kusini Unguja.

Na Othman Khamis Ame OMPR

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi alisema mwanachama wa CCM mwenye tabia ya kwenda kinyume na  Katiba pamoja na Muongozo wa chama hicho hafai na hana sifa za kuwa mwanachama wa chama.
 
Kauli hiyo  aliitoa wakati akikabidhiwa  rasmi ulezi wa Mkoa wa Magharibi Kichama kwa hatua ya kwanza  baada ya kutumikia wadhifa kama huo Katika Mkoa wa Singida  wakati akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri ya CCM Wilaya ya Dimani, Mfenesini na Mkoa Magharibi hapo katika Tawi la CCM Kiembe Samaki.
 
Balozi Seif alisema wapo baadhi ya Viongozi ndani ya Chama wenye tamaa ya fedha hasa wakati wa kampeni za uchaguzi na kukumbatia ubinafsi masuala ambayo kama yataachiliwa yanaweza kudhoofisha na hatimae kuvuruga nguvu za chama.
 
Mlezi huyo wa Mkoa wa Magharibi Kichama alionya kwamba chama cha  Mapinduzi hakitasita wala kuvumilia kuona baadhi ya watu hasa Viongozi wanakuwa wanafiki ndani ya chama hicho.
Balozi Seif alifahamisha kwamba suala liliopo mbele ya Viongozi na wanachama hao wa ccm hivi sasa ni kuimarisha Umoja na Mshikamano uliopo utakaosaidia nguvu ya Chama katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

 
Alieleza kwamba chama cha Mapinduzi ndio muhimili mkuu wa amani Nchini Tanzania hivyo ushindi wa chama hicho ni wa lazima katika kuilinda amani  hiyo kwa gharama zozote zile.
 
“ Katiba ya chama cha Mapinduzi iko wazi ikieleza wakati wa uchaguzi ukifika CCM lazima ishinde. Sasa azma hii itafikiwa vyema iwapo baadhi ya Viongozi  na wanachama wenye kasoro  ndani ya Uongozi wanajirekebisha mara moja “. Alisisitiza Mlezi hyo wa Mkoa Magharibi Kichama.
 
Balozi Seif aliwakumbusha Viongozi hao wa chama mkoa magharibi kwamba wana kazi kubwa mbele yao katika kuimarisha na kutetea hadhi na nguvu ya chama chao.
 
“ Leo nimekuja kuripoti kazi Mkoa wa Magharibi nikitokea Mkoa wa Singida Kichama. Natarajia niko katika mikono salama ya Uongozi. Nimefarajika kuja kulea Mkoa huu wa Magharibi ingawa Kamati Kuu ya CCM ilikuwa imeshaniteua kuendelea na ulezi Mkoani Singida “. Alieleza Balozi Seif.
 
Aliwasisitiza Viongozi hao kuhakikisha wanatoa Elimu kwa wanachama, wananchi na hasa Vijana katika kuelewa umuhimu wa kuendelea kukiunga mkono chama cha Mapinduzi chenye muelekeo wa kustawisha maendeleo ya Watanzania.
 
Akizungumzia suala la Rasimu ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Seif aliwakumbushaWajumbe wa Mabaraza ya Katiba Wilaya kupitia CCM kuhakikisha wanaichambua kwa makini na upeo zaidi kwa kuzingatia muongozo wa Chama chao.
 
Alisema Chama cha Mapinduzi kinaendelea kutoa hoja ya wazi katika mjadala huo wa Rasimu ya Katiba ya kuwepo kwa Katiba itakayozingatia mfumo wa Utawala wa Serikali ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Mapema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Yussuf Mohd Yussuf alimthibitishia mlezi huyo wa Mkoa Magharibi Kichama Balozi Seif kwamba Uongozi wa Chama Mkoani humo utampa nguvu ya ushirikiano katika kutekeleza jukumu lake.
 
Mwenyekiti Yussuf alisema zipo changamoto kadhaa katika utekelezaji wa majukumu ya Viongozi lakini zitashughulikiwa ipasavyo ili kuleta ufanisi ndani ya Chama na Taifa kwa ujumla.
 
Wakichangia katika kikao hicho baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri ya CCM wa Wilaya za Dimani, Mfenesini na Mkoa Magharibi walisema Chama kinaweza kuvurugika kama Viongozi watakwepa  kuitumia vyema Katiba na Kanuni za maadili ya Chama cha Mapinduzi.
 
Walisema tabia ya muhali inayotumiwa na Baadhi ya Viongozi katika kuchelewesha kutoa adhabu za  kisheria dhidi ya kiongoni au mwanachama aliyekiuka maadili inaweza kukiponza Chama na wanachama wake.
 
Chama cha Mapinduzi kimeamua kufanya mabadiliko ya mfumo wa Mikoa Kichama na hivi sasa uliokuwa Mkoa wa Mjini Magharibi  umegaiwa mikoa miwili Kichama ikitambulika kama Mkoa wa Mjini wenye Wilaya za Mjini na Amani wakati  Mkoa wa Magharibi una Wilaya za Dimani na Mfenesini Kichama.
 
Wakati huo huo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif alikabidhi mchango wa shilingi Milioni 1,000,000/- kusaidia ununuzi wa Mabati kwa ajili ya uwezekaji wa Tawi la CCM la Kijiji cha Kilima Matange  liliopo ndani ya Jimbo la Muyuni Mkoa Kusini Unguja.
 
Akikabidhi mchango huo kwa Katibu wa Tawi hilo Nd. Juma Mussa Haji hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kufuatia ahadi aliyoitoa mwezi wa Tatu mwaka huu  wakati wa ziara yake Mkoa wa Kusini Unguja Balozi Seif alisema sera ya CCM  ni kuwa na Ofisi za kisasa zenye hadhi ya Chama hicho.
 
Akitoa shukrani kwa niaba ya ujumbe ulioambatana kupokea mchango huo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kusini  Abdull aziz Hamad amempongeza Balozi Seif kwa juhudi zake za kusimamia vyema ilani na sera za Chama cha Mapinduzi.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>