Mbunge wa Jimbo la Rahaleo Mhe Abdallah Juma Mabodi, akimkabidhi Kombe la Ubimgwa Michuano ya Vijana Wasioowa na Walioowa Nahodha wa timu ya Wasioowa Ndg, Salum Mohammed, baada ya timu yake kushinda kwa mabao 2--0, mchezo uliofanyika uwanja wa lumumba.
Wawaaa Kombe letu
Mbunge wa Jimbo la Rahaleo Mhe Abdallah Juma Mabodi, akimkabidhi kleti ya soda ya Shani Nahodha wa timu ya Wasioowa Ndg. Salum Mohd.
Nahodha wa timu ya Walioowa akisalimiana na Viongozi baada ya kukabidhi mipira ya Ushindi wa Pili wa michuano hiyo.na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe. Nassor Salim Jazira. katikati na wa mwishi ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Abdallah Juma Mabodi.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Walioowa baada ya mchezo huo kumalizikwa kwa kufungwa mabao. 2--0.
Wachezaji wa timu ya Wasioowa wakiwa katika picha ya pamoja na wapenzi wao baada ya kukabidhiwa Kombe lao na Mbunge wa Jimbo la Rahaleo Mhe. Abdallah Juma Mabodi, akiwa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Nassor Salim Jazira.
Mambo ya Mbwa kachoka hayoo katika viwanja vya lumumba wakisherehesha katika viwanja hivyo.Washabiki wa timu ya Walioowa wakishangilia baada ya mchezo huo kumalizika kwa ushindi wa 2--0.
Mwakilishi wa Jimbo la RahaleoMhe. Nassor Salim na Katibu Mwenezi wa CCM Jimbo la Rahaleo wakifuatilia mchezo huo katika viwanja vya lumumba.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika fainali ya Wachezaji wa Timu ya Rangers ya Makadara walioowa na wasioowa, Watoto hawa ni wechezaji wa kesho wakishangilia mchezo huo.
Wapenzi wa mchecho wa Soka wakifuatilia mchezo huo katika viwanja vya lumumba.Beki wa timu wasioowa akijiandaa kumzuiya mchezaji wa timu walioowa mwenye jezi nyeupe, katika mchezo wa fainali ya kusherehekea miaka 50 ya Muungano na kuhamasisha Vijana kuacha matumizi ya dawa za kulevya kuepuka maambukizo ya Ukimwi Zanzibar.
Mchezaji wa Timu ya Walioowa akijaribu kumpita beki wa timu ya Wasioowa, wakati wa mchezo huo wa kusherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanzania uliofanyika katika viwanja vya lumumba, timu ya Wasioowa wameshinda 2--0.
Mshabiki wa timu ya Ranfers wasioowa akishangilia timu kwa ushindi wa bao 2--0 dhidi ya timu Walioowa, mchezo uliofanyika katika viwanja vya lumumba akifurahia ni Mbunge wa Rahaleo Dkt. Juma Abdallah Mabodi.