Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wakifuatilia Mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdurahaman Kinana, akihutubia katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibanda maiti kuhutubia wananchi kuhusiana na Uuundwaji wa Katiba Mpya. Tanzania.
Dkt. Emmanuel Nchimbi, akisoma kitabu cha Maalim Seif Shariff alichotunga, kinachoelezea Muungano na hali ya Ulinzi na Usalama.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Ummy Mwalimu akitowa dozi katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi, kuelezea mwenendo wa Bunge la Katiba.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Salmin Awadh, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar.
Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya mkutano kibanda maiti wakifuatilia Mkutano wa hadhara
Wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano huo.
Muungano wa Serekali Mbili
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Makamu Mwenyekiti wa UWT Mhe. Asha Bakari, akihutubia katika mkutano huo na kutowa maelezo kuhusiana kuimarisha Muungano wa Serekali mbili.
Viongozi wa meza Kuu wakifuatilia mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM,katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar.
Mbunge wa Mtera Mhe.Livingstone Lusinde, akihutubia katika mkutano huo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi, akihutubia katika mkutano wa hadhara ulioafanyika katika viwanja vya kibanda maiti akihamasisha muundo wa Muungano wa Serekali mbili.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi, akisisitiza jambo katika mkutano wa hadhara.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia katika viwanja vya kibanda maiti wakati akihutubia Katibu Mkuu wa CCMMke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume akihutubia katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar akisisitiza jambo. na kuwataka Wazanzibar kudumisha Muungano na kuwaenzi Waashishi wa Muungano huo Mzee Karume na Mwalimu Nyerere. kwa kufanikisha muungano huu hadi leo miaka 50.
Mama Fatma Karume akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara kibanda maiti Zanzibar.
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi akifuatilia mkutano huo katika viwanja vya kibanda maiti Zenj.Wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano huo.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia kwa aina yake katika viwanja vya kibanda maiti wakati akihutubia Katibu Mkuu wa CCM.
Mjumbe wa Bunge la Katiba na Mwakilishi wa Kwamtipura Mhe. Hamza Hassan akihutubia katika mkutano huo akiwa na kopi ya Muungano iliosainiwa na Waasisi wa Muungano huo Mzee Karume na Mwalimu Nyerere. uliowasilishwa katika mkutano wa Bunge la Katiba Dodoma.
Mjumbe wa Bunge la Katiba Mhe. Steven Wasira wakihutubia katika mkutano huo uliohudhuriwa na Wanachama wengi bila ya kujali mvua iliokuwa ikinyesha katika kiwanja hicho cha kibanda maiti.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye, akiwahutubia wananchi na WanaChama wa CCM katika viwanja vya kibanda maiti.
Viongozi wa Meza Kuu wakinyoosha mikono juu kuashirika kuunga mkono Muungano wa Serekali Mbili, katika Uundwaji wa Katiba Mpya ya Tanzania.
Wananchi wakiuunga mkono muundo wa Muungano wa Serekali Mbili wakiwa katika viwanja vya Kibanda maiti.