Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Bajeti bilioni 705 SMZ

$
0
0
Na Mwandishi Wetu.
SERIKALI imetangaza bajeti ya shilingi bilioni 705.1 kwa mwaka wa fedha 2014/2015, ambapo shilingi bilioni 399.8 zinatokana na mapato ya ndani na shilingi bilioni 305.3 ni mapato ya nje na misaada.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Vuga, Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee, alisema serikali inatarajia kutumia jumla ya shilingi bilioni 374.7 kwa shughuli za kawaida zikiwemo bilioni 184.5 fedha za mishahara ya wafanyakazi wa umma.

Alisema viwango vya mishahara hiyo vinakwenda sambamba na mabadiliko ya mishahara kulingana na viwango vya elimu na uzoefu kwa watumishi wa umma.

“Kila mfanyakazi atapata mshahara uliofanyiwa marekebisho kwa mujibu wa elimu na uzoefu wake,” alisema.

Alisema bajeti ya mwaka huu imeangalia vipaumbele vikuu vinne, ambavyo ni afya, miundombinu, maji safi na elimu ambapo jumla ya shilingi bilioni 159.6 zikiwa sawa na asilimia 48.4 ya bajeti ya maendeleo, zinatarajiwa kutumika kwa miundo mbinu ya uwanja wa ndege ukiwemo ujenzi wa bara bara za kurukiwa ndege, kukamilishwa kwa maegesho pamoja na kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa ndege Pemba.

Alisema shilingi bilioni 30.6 ambazo ni sawa na asilimia 9.3 ya bajeti ya maendeleo ya zinatarajiwa kutumika katika sekta ya afya, ambapo elimu itatumia bilioni 28.4 sawa na asilimia 8.6 ya fedha za maendeleo.

Alisema serikali pia imezipa kipaumbele huduma za maji safi na salama ambapo inatarajia kutumia shilingi bilioni 26.8 sawa na asilimia 8.1 ya bajeti na kuongeza kuwa, sekta hizo zinachangia maendeleo na ukuaji wa uchumi wa nchi.


Kuhusu mchango wa serikali kwa mwaka huu wa fedha, alisema serikali ilichangia shilingi bilioni 65.6 ambapo washirika wa Mmaendeleo walichangia milioni 264.

Akizungumzia suala la mfumko wa bei, alisema umeshuka kwa asilimia 9.4 hadi mwaka 2012 ambapo kwa mwaka 2013 ulikuwa asilimia 5, hali iliyotokana na mpango wa serikali kupunguza kodi katika bidhaa za vyakula vikiwemo mchele, sukari na ngano hasa kwa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Aidha alisema uzalishaji wa mpunga ulichangia ukuaji wa uchumi ambapo serikali inaendelea kudhibiti bei za vyakula zisipande.

Katika kupunguza ajira kwa vijana nchini, alisema sekta ya uwekezaji ilizidi kwa mwaka 2013 ambapo ZIPA ilisajili  miradi 35 iliyozalisha ajira 1365 wakati mwaka 2012 miradi 25 ilisajiliwa na kuzalisha ajira 1,123 jambo ambalo lilikuza ajira kwa vijana hasa katika sekta binafsi.

Akizungumzia kukua kwa pato la taifa alisema hadi mwaka 2013 lilikuwa shilingi bilioni 1442.8 wakati mwaka 2012 lilikuwa 1342.6 bilioni.

Hata hivyo alisema bajeti ya mwaka huu imezidi kwa asilimia 7.1 ikilinganishwa na ya mwaka jana ambapo ilikuwa bilioni 658.5 kati ya fedha hizo bilioni 380.6 zilikuwa fedha za nje na bilioni 277.9 zilitokana na mapato ya ndani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>