Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mgimwa, Ridhiwani waapishwa

$
0
0

Na Fatina Mathias, Dodoma
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana linaanza kikao chake cha bajeti ambapo muda wa kuchangia na kuwasilisha bajeti za Wizara   mbalimbali ukiwa umepunguzwa.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa shughuli za bunge, John Joel, alisema, muda wa kuchangia bajeti hiyo umepunguzwa kutoka dakika 10 hadi saba na muda wa uwasilishaji wa bajeti za Wizara ukiwa umepunguzwa.

Alisema kutokana na mabadiliko hayo sasa kila wizara itapewa siku moja ya kuwasilisha bajeti yake na kujadiliwa.




“Tumepima muda tukaona unatosha,” alisema.
Aidha alisema bunge litaanza kujadili hotuba ya bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu leo jioni (jana) kuanzia saa kumi.
Alisema bunge hilo pia limeongeza siku za kufanya kazi na litakaa mpaka siku za Jumamosi lengo likiwa ni kuokoa muda uliopotea.
“Vikao vitaanza saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana na kutakuwa na mapumziko ambapo vitaanza tena saa 10 hadi saa mbili usiku na kwa siku za Ijumaa vikao vitaanza saa tatu hadi saa saba na Jumamosi vitaanza saa tatu mpaka saa saba,” alisema.

Alisema, bunge hilolitaendelea hadi tarehe Juni 27.
Pia alisema kwa mujibu wa ratiba bajeti inaweza kusomwa Juni 12, mwaka huu.
Katika kikao cha jana, wabunge wawili wapya Ridhiwani Kikwete na Godfyey Mgimwa, waliapishwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kuwa wabunge.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>