Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mapigano yajeruhi 14

$
0
0
Na Francis Rikanga, ARUSHA
WATU 14 wa kijiji cha Engalaoni kata ya Mwandet mkoani Arusha, wamepigwa na kujeruhiwa vibaya na kikundi cha watu wanaosadikiwa wanatoka wilaya ya Monduli, waliovamia na kujenga makazi katika maeneo ya malisho yaliyotengwa na wafugaji wa wilaya ya Arumeru kwa ajili ya malisho ya mifugo.

Watu hao walishambuliwa kwa sime, mikuki fimbo na marungu na wamelazwa hospitali ya Selian mkoani Arusha na baadhi yaokuruhusiwa huku mmoja wao akiwa katika hali mbaya.

Akizungumza na waandishi wa habari kijijijini hapo, Diwani wa kata ya Mwandet, Bonifas Mollel, alisema watu hao walijeruhiwa na kikundi cha watu kutoka wilaya ya Monduli.

Aliwataja watu hao kuwa ni Melau Taiko, Muyae Kuresoi, Lengai Kivuyo, Mepalaari Kuresoi, Lomnyak Meijo,  Akui Lomeji na Isack Lesikar.

Wengine ni Loitore Lomeji, Balozi Kapurwa, Moiyo Kapurwa, Shiiki Korduni, Losieku Kimani, Taiko Kuresoi na Kooki Sane, ambaye hadi sasa amelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa vibaya kichwani na kukatwa vidole vinne vya mkono wa kulia.


“Kwa kweli serikali haina budi kukidhibiti kikundi hiki, watu wanapigwa kama wanyama. Huyu mzee Kooki Sane amepigwa vibaya, kichwa hakifai, tumboni hadi kifuani amechomwa na mkuki na amekatwa vidole vinne vya mkono wake wa kulia, watu hawa ni lazima serikali sasa iwadhibiti,” alisema.

Aidha, alisema pamoja na watu hao kupigwa na kujeruhiwa, maboma yao yamechomwa moto na mifugo kuteketezwa na kusababisha hasara kubwa huku mifugo mingine ikiibiwa.

Alisema katika maboma 35 yaliyochomwa, ndama 12, mbuzi 30, dawa za mifugo, nguo na vyombo mbalimbali vya wafugaji navyo viliteketezwa.

Aidha, alisema tokea watu hao wavamie maeneo hayo, mifugo 103 na punda 26 wameibiwa.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi ulibaini kuwa vurugu hizo zimekuwa zikitokea mara kwa mara na chanzo ni watu wa Monduli kuzuia mifugo ya wilaya ya Arumeru kuingia katika maeneo ya malisho pamoja na kuwa maeneo hayo ya malisho yapo ndani ya wilaya ya Arumeru.


Katibu wa Umoja wa Wafugaji wa wilaya ya Arumeru, Yohanes Emanuel Lomanyaa, alisema mipaka ya wilaya ya Aumeru iko wazi na tayari wamemtembeza mkuu wa wilaya ya Arumeru kukagua mipaka hiyo.  

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>