Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Z’bar hatua chache kuacha utegemezi wa umeme

$
0
0

UMOJA wa Ulaya (EU) umekubali kuisaidia Zanzibar katika upatikanaji wa nishati ya umeme, inayotokana na nguvu za jua na upepo.

Mradi huo mkubwa wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, utatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, chini ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), lenye dhamana ya kuwasambazia umeme wananchi wa Zanzibar.

Mradi huo utahusisha masuala ya utafiti na utekelezaji wa mradi huo, hadi nishati hiyo itakapopatikana ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia kupunguza utegemezi wa umeme.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini utekelezaji wa mradi huo, Balozi wa Umoja wa Tanzania na kanda ya Afrika Mashariki, Filiberto Ceriani Sebregondi, alisema lengo la mradi huo ni kukuza maendeleo endelevu na kupunguza umaskini kwa wananchi wa Zanzibar.

Alisema mradi huo unatekelezwa kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya Zanzibar na Umoja huo uliodumu kwa muda mrefu sasa.

Alisema mradi huo utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa Zanzibar na wananchi wake.
Aidha alisema, EU itaendelea kuisaidia Zanzibar na Tanzania kwa jumla katika sekta mbali mbali za kiuchumi, ambapo kuanzia mwaka huu hadi 2020 umoja huo utatoa dola za Marekani milioni 626.


Nae Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee, aliipongeza EU kwa kusaidia sekta ya nishati ili kuhakikisha Zanzibarinakuwa na vyanzo vyake vya umeme.

Aidha aliishukuru EU kwa kuendelea kuiunga mkono Wizara ya Fedha, katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kiuchumi kwa faida ya nchi na wananchi wake.

Nae Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati, Ramadhan Abdalla Shaaban,alisema mradi huo utasaidia kasi ya upatikanaji wa nishati ya umeme, ambapo kwa muda mrefu Zanzibarimekuwa ikichukua juhudi kuhakikisha inapatikana.

Katika hatua nyengine, EU imesaini mkataba wa kuzisaidia asasi mbali mbali za kiraia (NGO’s) zilizochini ya mwamvuli wa ANGOZA zinazoshiriki katika utetezi wa haki za binaadamu.

Mradi huo wa miaka mitatu, utasaidia kupunguza kasi ya udhalilishaji wa wanawake na watoto, kupunguza tatizo la ajira kwa watoto, kuimarisha demokrasia na utawala bora na kulinda haki za binaadamu na usawa wa kijinsia.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8 utatekelezwa Unguja na Pemba.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Sheria na Katiba, Aboubakary Khamis Bakary, alisema asasi zitakazofaidika na fedha hizo ni zile zinazofanya shughuli zake na ambazo zimepata usajili kwa mujibu wa sheria.
Mwenyekiti wa ANGOZA, Asha Aboud Mzee, alisema msaada huo umeweka uhusiano mwema kati ya NGO’s, serikali na Umoja wa Ulaya na kwamba ni faraja kubwa kwa asasi za kiraia nchini.

Katika mkataba wa radi wa nishati ya umeme, serikali iliwakilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Khamis Mussa Omar na mradi wa kusaidia NGO’s serikali iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Juma Ameir Khafidh.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>