Na Andrew Chale
MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin kufuatia kufanya vizuri hivi karibuni katika onyesho kubwa la mavazi ya ubunifu lililokuwa maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Abuja, Nigeria, huku asilimia kubwa kwenye jukwaa hilo akitumia vazi lililonakshiwa alama za bendela ya Tanzania, ‘National colours Asia idarous's design’ tayari watu mbalimbali duniani wameombwa kutengenezewa mtundo huo.
Akizungumza jiini Dar es Salaam, na mtandao huu, Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, alisema kuwa watanzania na raia mbalimbali wa kigeni duniani kote wametoa order za kutengenezewa vazi kama hilo ambalo kwa asilimia kubwa limekuwa ni kivutio huku likimweka mtu yoyote katika hali ya ubora na kupendeza.
Vazi hilo ambalo linabamba ikiwemo aina ya kitambaa maalum na skafu kubwa inayopachikwa kifuani yenye nakshi ya alam za Taifa, pia tokea kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye televisheni nchini Nigeria na Ulala, imekua gumzo kubwa kwa sasa huku wengine wakishahuri liingizwe kwenye tukio la kusaka vazi la Taifa.
“Kwa sasa nipo katika kushughulikia oda za wateja wangu ambao wengi wapo Mataifa ya kigeni ikiwemo Nigeria, Ghana, Kenya, uingereza, Marekani na kwingineko pamoja na Tanzania” alisema Aisa Idarous.
Alisema kuwa, vazi hilo ambalo pia siku ya onyesho hilo karibu wageni wote wakiwemo balozi wan chi zaidi ya 61 zilizohudhulia siu hiyo ya Muungano nchini Nigeria, zilivutiwa na hata kulipongeza kutokana na ua kielelezo cha Utaifa la Tanzania.
Aidha, Asia Idarous alisema kuwa, matilio ya vazi hilo yapo yanayotoka nchini Tanzania namengine nje ya nchi ikiwemo Nigeria, tayari baadhi hoda zimekamilika na baadhi ameanza kuziuza katika duka la Fabak fashions lililopo Mikocheni mkabara na Kwa Mwalimu Nyerere.
“Hii ni heshima kwangu na kwa Tanzania, kwani vazi hili limeokea kukubalika duniani kote na kupelekea kuwa utambulisho maalum wa Mtanzania. Vazi hili kwa kawaida anavaa mtu yoyote na kwenye tukio lolote lile na hata kumweka mtu katika hali ya umaridadi, ikiwemo kwa wanaume na wanawake” alisema Asia Idarous.
Asia Idarous pia aliwataka kwa watu watakao taka kuagiza ama kutoa order, wanaweza kumpigia +255713263363, ama dukani kwake Fabak fashions Mikocheni kwa Mwl. Nyerere.