Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mangula: Wanaoisaliti CCM kushughulikiwa

$
0
0
Na Fatina Mathias, Dodoma
Wanachama wa CCM waliokisaliti chama wakati wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga na Chalinze watachukuliwa hatua.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Philip Mangula, katika hafla ya kuwapongeza Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa.

Alisema kwa mujibu wa kanuni za CCM kosa kubwa kuliko yote ni kwa mwanachama kukisaliti chama hicho kwa kushirikiana na upinzani kwa lengo ya kukiweka katika hali ya kushindwa.

Alisema watachukua hatua kwa wanachama wote walioshirikiana na upinzani kupinga uteuzi wao na kwamba makatibu kata wanajua hatua zitakazochukuliwa.


Aliwataaka wabunge hao kuepuka makundi ndani ya majimbo yao kwa kuwa kanuni za CCM  zinapiga marufuku kwa kiongozi kujenga makundi yanayoweza kuvunja umoja ndani ya chama.

Aidha, alipiga marufuku kwa mwanachama yeyote kusogeza pua yake kwa nia ya kuanza kupiga kampeni katika majimbo hayo ambayo tayari yana wabunge.

Alisema wabunge hao waachwe wafanye kazi zao katika kipindi hiki kilichobaki na kwamba wanachama wanaruhusiwa kutangaza nia lakini ni marufuku kuanza kampeni.

“Marufuku kutangaza nia kabla ya wakati, muda wa kampeni utatangazwa rasmi, makatibu wa wilaya  simamieni hili, atakayefanya kampeni kabla ya wakati mwekeni katika kumbukumbu ya uhalifu,” alisema.

Alisema ni marufuku kwa  mwanachama asiye kiongozi katika eneo husika kutoa msaada, mchango au zawadi katika eneo analokusudia kugombea.

Kwa upande wake, Ridhiwani alisema CCM imemlea tangu akiwa na miaka minne na kuahidi hatakiangusha chama hicho.


Naye Mgimwa aliahidi kufanya kazi ya ubunge kwa maslahi ya taifa na jimbo la Kalenga.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>