Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

SMZ yaahidi kumaliza tatizo la ajira

$
0
0
Na Mwashamba Juma
SERIKALI imeandaa mikakati madhubuti kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana linalorudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Tatizo hilolimewasababishia vijana wengi kuwa tegemezi kwa kushindwa kubuni mbinu za kujikwamua na ugumu wa maisha jambo ambalo hurudisha nyuma juhudi zao katika kujikwamua kimaendeleo.

Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi, Fatma Gharib Bilali, aliyasema hayo katika ukumbi wa Salama Bwawani, wakati akifunga kongamano la vijana lililokuwa likijadili mpango mkakati wa ajira kwa vijana Zanzibar.

Alisema suala la ajira kwa vijana sio tu chanagamoto inayoikabili serikali ya Zanzibarbali ni tatizo la dunia nzima ambapo moja ya jitihada za serikali ni kuandaa kongamano la vijana lililowapa fursa ya kutoa mawazo kwa serikali na kujadili pamoja na kutoa mawazo ya kukabiliana na changamoto hizo.

“Kongamano hili ni juhudi za serikali ya Zanzibar katika kuwapatia fursa za ajira vijana wake ili kujikwamua na maisha,” alisema.

Alisema kongamano hilo limetoa fursa kwa vijana kutoa maoni yao juu ya kuboresha rasimu ya mpango mkakati wa ajira kwa vijana wa  Zanzibar ya mwaka 2014/ 2019 pamoja na kuwataka vijana kuiga mifano ya wenzao waliothubutu na kuweza kukabiliana na changamoto za ajira nchini.

Alisema serikali kupitia wizara yake, itahakikisha kuyafanyia kazi mapendekezo na michango iliyowasilishwa kwenye mpango mkakati huo, sambamba na kufanya jitihada za kuwapatia vijana wake ajira zenye staha.

Aidha alisema kongamano lilianisha fursa za ajira kwa vijana hasa kwenye sekta ya kilimo, biashara, utalii na ujasiriamali kupitia vyama vya ushirika na vyuo vya amali.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kazi Duniani kanda ya Afrika Mashariki, Alex Musindo, alisema ILO limekuwa likitoa kipaumbele kwa serikali ya Zanzibar katika kuipatia fursa za upatikananaji wa ajira kwa vijana.


Alisema ni jukumu la wote kutekeleza mpango mkakati wa ajira kwa vijana na kuufanya kuwa endelevu kwa maendeleo ya nchi na mustakbali wa vijana katika kujikwamua na ugumu wa maisha.

Akizungumzia suala la ujasiriamali kwa vijana, Mkurugenzi huyo alisema ujasiriamali sio suluhisho pekee la kutatua changamoto za ajira kwa vijana, bali ni sehemu ya biashara na kuongeza kuwa taasisi za umma, serikali pamoja na ajira binafsi zina wajibu wa kuwagomboa vijana na janga la uhaba wa ajira.

Nae Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama huru vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC), Khamis Mwinyi wakati akizungumzia sheria za utekezaji wa sheria hiyo, alisema bado haisimamiwi ipasavyo na kutoa mwanya kwa wageni kuchukua nafasi za wazawa jambo ambalo huwasababishia vijana kukutana na hali ngumu ya ukosefu wa ajira.

Alisema taasisi yake inahakikisha mazingira bora ya kazi kwa wafanyakazi sambamba na kuendeleza jitihada za kupigania maslaahi ya kazi zao.

Alisema mpango mkakati wa ajira kwa vijana, unaenda sambamba na vipaumbele vya mikakati ya kimataifa ya kuhakikisha ajira kwa vijana duniani.

Alisema ZATUC kama sehemu ya ILO itahakikisha inatekeleza mikakati ya ajira kwa vijana Zanzibarkwa sasabu ongezeko la ajira kwa vijana linaimarisha vyama vya wafanyakazi.

Katibu wa Jumuiya ya Waajiri Zanzibar (ZANEMA), Salahi Salahi, alisema kongamato limewawezesha kujua matatizo na mafanikio ya vijana kutokana na tatizo la ugumu wa ajira kwa vijana ambalo serikali inakabiliana nalo.

Alisema vijana wana wajibu wa kuuliza na uendeleza mpango huo sambamba na kuwataka kuuliza juu mwendelezo wake kwa serikali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>