Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Watoto 948 waliungua moto 2012/2013

$
0
0
Na Laylat Khalfan
Idadi ya watoto wanaoungua moto inaongezeka kila mwaka, ambapo zaidi ya watoto 948 waliungua moto na kulazwa katika hospitali kuu ya Mnazimmoja katika kipindi cha mwaka 2012 na 2013.

Akizungumza kwa huzuni na mwandishi wa habari hizi,  Katibu wa hospitali hiyo, Hassan Makame Mcha, alisema watoto wanaoungua moto ni wale wenye umri wa kuanzia miezi sita ambao wako katika hatua ya kutambaa.

Alisema watoto hao walilazwa katika hospitali hiyo wakiwa na majeraha mabaya ya kuungua uji moto, maji, chain a wengine kuungua moto wenyewe.

Alisema chanzo cha watoto wengi kuungua moto, ni wazazi kutokuwa makini kuwaangalia watoto wao hasa katika hatua ya kutambaa.

Alisema akina mama wengi ni wazembe na wafuatilii nyenendo za watoto wao, ambao wanahitaji uangalizi wa karibu hasa wakati wa kutambaa ili kuondoa hatari ya kuungua na kuwasababishia makovu ya muda mrefu na wakati mwengine kupoteza maisha.


Alisema ili kukabiliana na wazazi wazembe, serikali haina budi kuanzisha kitengo maalum kitakachotoa adhabu kali kwa wazazi wazembe wasiowachunga watoto wao na kusababisha kuungua.


Aidha alisema ipo haja kwa wazazi kuwa makini na kuwachunga watoto wao hasa katika umri wa kutambaa ili kuwanusuru na matukio ya kuungua moto.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>