Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Auawa baada ya kuwadhulumu wenzake fedha za madini

$
0
0
Na Kadama Malunde,Shinyanga
Kijana mmoja aitwaye Mihangwa Maguta (30) mkazi wa kijiji cha Nyenze kata ya Mwadui-luhumbo wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga, ameuawa kwa kupigwa jiwe kubwa kichwani na wenzake watatu kutokana na kile kilichotajwa kuwa aliwadhulumu pesa za mauzo ya madini ya almasi.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Shinyanga, ACP Kihenya Kihenya, tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Nyenze kata ya Mwadui-Luhumbo wilayani Kishapu.

Alisema marehemu aliuawa kwa  kupigwa jiwe kubwa na wenzake kichwani na kumsababishia kifo chake papo hapo.

Kamanda Kihenya alisema marehemu na wenzake walikuwa wanafanya shughuli ya kuchimba madini ya almasi katika eneo la mgodi wa madini ya almasi Mwadui unaomilikiwa na Wiliamson na baada ya kupata madini  walimpa  mwenzao akayauze ili wagawane pesa.

Hata hivyo, marehemu baada ya kuuza madini hayo aliwadhulumu wenzake  na ndipo walipopandwa na hasira wakaanza kumshambulia kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na alipoanguka chini walibeba jiwe kubwa kwa pamoja na kumpiga nalo kichwani na kusababisha kifo.


Kamanda Kihenya alisema thamani ya pesa ya madini haijuliknani kutokana na watuhumiwa kutokujua thamani yake halisi, huku akitaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni kugombania mali.


Aliwataja watuhumiwa wa mauji hayo kuwa ni Makoye Mtemi (56), Abdallah Iddi (32) na Ally Omari (22) wote wakazi wa kijiji kimoja cha Nyenze wilayani humo na wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>