Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mtoto aua wazazi wake

$
0
0
Na Dixon Busagaga,Hai
Wanandoa wawili wameuawa kinyama baada ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yusuf Njau (32), anayeaminika kuwa ni mtoto wa kumzaa wa wanandoa hao, kuwakata kata kwa shoka kisha kuchoma moto nyumba  yao na kutokomea kusiko julikana.

Tukio hilo la kusikitisha na la aina yake limetokea juzi majira ya saa 12:30 jioni katika kijiji cha Masama-Roo,  kata ya Machame Mashariki,wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro baada ya kijana huyo kuchukua uamuzi huo kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Waliouawa wametambulika kwa majina ya Shahidu Njau(60) ambaye  ni baba yake mzazi na  Minae Swai (57) ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Halfani Swai, alisema walipofika katika eneo la tukio baada ya kusikia mayowe walikuta watu wakizima moto huku mwili wa mama mtuhumiwa ukiwa umelala chini.

Alisema wakati kijana huyo akiendelea kutenda unyama huo,alitokea baba yake mzazi, mzee Shaidu  aliyekuja kuingilia kati ugomvi wa mama na mwanae lakini naye alikatwa kichwani kwa shoka.

Alisema mwili wa baba ulikutwa ukiwa pembeni wa mwili wa mkewe ukiwa na majeraha ya shoka  kichwani.


Alisema walimchukua kwa nia ya kuokoa uhai wake lakini muda mfupi baada ya kutoka kwenye eneo la tukio wakiwa katika kituo cha mafuta maeneo ya Sadala Shaidu, alipoteza maisha.

Taarifa kutoka kijiji hicho zinasema muuaji, Yusuf Njau, ambaye amewahi kujifunza ngumi akiwa Dar es Salaam pia aliwahi kuwatishia uhai baadhi ya ndugu zake zaidi ya mara mbili.

Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa kijiji hicho, Halfani Swai, alisema kijana huyo ambaye ni mkorofi pia aliwahi kutishia kuwaua shangazi na baba mdogo.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa anatafutwa.

Alisema miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Hai.

Kwa upande mkuu wa wilaya ya Hai, Novatus Makunga, alisema tukio hilo ni la kinyama na kuwataka wananchi kuwa na subira huku akitahadharisha raia kutochukua hatua mikononi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>