Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Z’bar yakaribia kutekeleza adhabu ya kutumikia jamii

$
0
0
Na Amina Omari,Tanga
Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo kwenye hatua za mwisho za kupitisha sheria ya adhabu ya kuitumikia jamii kwa watoto wenye umri wa miaka 18, wanaopatikana na hatia na kuhukumiwa vifungo.

Hayo yamaeelezwa na Mkurungezi wa Maendeleao ya Wanawake na Watoto, Rahma  Ali Khamis,wakati akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wakufunzi wa kitaifa kuhusiana na malezi kwa familia kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika jijini Tanga.

Alisema kukamilika kwa sheria hiyo kutatoa mwanya kwa watoto kurekebishwa tabia zao na jamii badala ya kuwachanganya kwenye magereza ya wakubwa.

Alisema katika kukabiliana na tatizo la ukatili kwa watoto na wanawake hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa ikiwemo kutoa elimu kuhusu madhara ya vitendo hivyo pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria watuhumiwa wa vitendo hivyo.


Aliongeza kuwa kuanzisha mahakama za watoto ambazo zina mahakimu wake na wanasheria wake kumesaidia kuleta msaada wa kisheria kwa watoto hao.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe, ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliviagiza vyuo vya maendeleo ya jamii pamoja na vyuo vya wananchi kuingiza kwenye mtaala masula ya elimu ya malezi ili wanafunzi wanaomaliza watoke na uwelewa kuhusu jinsi ya kuzuia ukatili.


Alisema mitaala hiyo itasaidia kupunguza tatizo la unyanyasi wa kijinsia wanaofanyiwa watoto katika maeneo mbalimbali kwani elimu hiyo itawafikia watu wengi katika jamii hususani madhara ya ukatili huo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>