Wanakijiji wa Kijiji cha Maisha Plus ambao ni Vijana wa Maisha Plus pamoja na Mama shujaa wa Chakula wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster ambaye hayupo
Kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster, Mkamiti Mgawe wa Oxfam na Babu kutoka kijiji cha Maisha Plus Rajabu Msumi wakiongea na washiriki wa Maisha Plus na Mama Shujaa wa Chakula.
Mkamiti Mgawe wa tatu kutoka kushoto akimtambulisha Markia wa Kijiji cha Maisha Plus kwa Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster
Mkurugenzi wa Maisha Plus akioneshwa Shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanakijiji wa Kijiji cha Maisha Plus
Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akioneshwa moja ya jiko lililotengenezwa na Akina mama Shujaa wa Chakula pamoja na Vijana wa Maisha Plus.
Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akioneshwa moja ya Ghala la kienyeji na imara kwa ajili ya kuhifadhia vyakula.
Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akioneshwa shamba linalotumia kilimo hai na cha kisasa katika kijiji cha Maisha Plus ambapo wahusika wa shughuli hizo na uangalizi wa Shamba hilo ni Mama Shujaa wa Chakula na Vijana washiriki wa Maisha Plus
Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiendelea na ziara yake ndani ya kijiji cha Maisha Plus na kujionea mambo mbalimbali yanayo endelea Kijijini hapo.
Chereko na vifijo vilitawala katika kijiji cha Maisha Plus kuonyesha furaha kwa kuwa Katika siku hii kijiji kilitembelewa na Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiongozana na mfanyakazi wa Oxfam Mkamiti Mgawe ili kujionea miradi mbalimbali waliyobuni wanakijiji cha Maisha Plus.
Mkurugenzi alifurahishwa sana na kazi zilizofanywa kwa usatadi na umahiri wa hali ya juu na kujionea hazina za vipaji vya wanakijiji hao. Oxfam Tanzania ni moja ya wadhamini na wadau wakuu wa Maisha Plus na Mama Shujaa wa Chakula 2014.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja ya utengenezaji wa batiki, sabuni, kikapu cha ajabu, bustani ya kuhama, jiko la gesi, aina mbalimbali za majiko ya udongo wa mfinyanzi, ufugaji bora wa kuku na nyuki, bustani za mboga na shamba linalotumia kilimo hai na kilimo cha kisasa.
Chereko na vifijo vilitawala katika kijiji cha Maisha Plus kuonyesha furaha waliyonayo na pia kusherehekea siku ya mama duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 11 Mei. Katika siku hii kijiji kilitembelewa na Mkurugenzi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiongozana na mfanyakazi wa Oxfam Mkamiti Mgawe kujionea miradi mbalimbali waliyobuni wanakijiji cha Maisha Plus.
Mkurugenzi alifurahishwa sana na kazi zilizofanywa kwa usatadi na umahiri wa hali ya juu na kujionea hazina za vipaji vya wanakijiji hao.
Oxfam Tanzania ni moja ya wadhamini na wadau wakuu wa Maisha Plus na Mama Shujaa wa Chakula 2014. Miradi iliyotembelewa ni pamoja ya utengenezaji wa batiki, sabuni, kikapu cha ajabu, bustani ya kuhama, jiko la gesi, aina mbalimbali za majiko ya udongo wa mfinyanzi, ufugaji bora wa kuku na nyuki, bustani za mboga na shamba linalotumia kilimo hai na kilimo cha kisasa.