Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Balozi Seif Ali Iddi akutana na Ujumbe wa Kampuni ya Kijani Agro Limited ya Israel.

$
0
0
Mwakilishi wa Kampuni ya Kijani Agro Limited ya Nchini Israel Bwana Ronen Almog akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Ronen Almog akimuonyesha Balozi Seif baadhi ya Vitabu vyenye maelezo ya miradi inayotekelezwa na Kampuni ya Kijani Agro Limited.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Kapumi ya Kijani Agro Limited Bwana Ronen Almog aliyepo kati kati kuhusu suala la sekta ya kilimo ambayo kampuni hiyo inajishughulisha nayo.Pembeni yao ni Mjumbe wa Kampuni hiyo aliyeambatana na Bwana Ronen Almog Bibi Rebbeca Saroju.Picha na Hassan Issa wa – OMPR




Kampuni `ya Kijani ya Agro Limited yenye Makao Makuu yake Nchini Israel  imejitolea kuanzisha Kilimo cha mazao ya mbatata na Vamila kwa kutumia mfumo wa teknolojia ya kisasa utakaoshirikisha Vijana wazalendo hapa Zanzibar.
Uongozi wa Kampuni hiyo pia umejipanga kutoa mafunzo maalum kwa Vijana katika sekta ya Kilimo kwa kuwajengea uwezo wa uzalishaji wa mazao tofauti yatakayowapa fursa ya ajira badala ya kusubiri ajira ya Serikali.

Mwakilishi wa Kampuni hiyo ya Kijani Agro Limited yenye Tawi lake Jijini Dar es salaa na Mkoani Iringa Bwana Ronen Almog alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwa Balozi  Vuga Mjini Zanzibar.

Bwana Ronen Almog alisema uwepo wake Nchini Tanzania ndani ya kipindi cha miaka saba akijishughulisha na shughuli za Kilimo pamoja na utoaji wa mafunzo ya sekta hiyo Mkoani Irringa alisema Zanzibar imebarikiwa kuwa na eneo zuri la Kilimo licha ya udogo wa ardhi yake.


Alisema Uongozi wake utajitahidi kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo katika kuona ushiriki wa Wananchi hasa wakulima katika kupata Taaluma ya kilimo itakayotolewa na wataalamu wa Kampuni hiyo unafanikiwa vyema.

Alieleza kwamba Kituo maalum cha mafunzo ya Kilimo Kitaanzishwa  ili kuwapa fursa kubwa wakulima na hasa Vijana kujifunza mbinu za kisasa za Kilimo kwa lengo la kuendeleza sekta hiyo katika mfumo wa kiteknolojia.

“Ndani ya mipango yetu Tumefikiria kujenga Kijiji cha Vijana { Yourth Village } hapa Zanzibar katika kuona kundi kubwa la wananchi wasiokuwa na ajira wanajiwezesha kwa kuitumia Sekta ya Kilimo “. Alisema Bwana Ronen.

Mwakilishi huyo wa Kampuni ya Kijani Agro Limited alifahamisha kwamba Taasisi yake tayari imeshawekeza katika mradi wa Kilimo katika Mikoa ya Dodoma na Iringa hatua ambayo imechangia ongezeko la uzalishaji wa mazao ya Nafaka na mboga mboga.

“ Tayari tuna zaidi ya Hekta 650  za mboga mboga mkoani Iringa zinazohudumiwa kitaalamu na kutoa mazao yaliyo katika kiwango kinachokubalika  kimataifa “. Alieleza Bwana Ronen.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Kilimo bado kitaendelea kuwa sekta mama kwa uchumi wa Zanzibar ambacho hutoa ajira kwa  zaidi ya asilimia 70%.

Balozi Seif alisema Mbatata na Vanila  ni mazao yanayohitajika zaidi hapa Zanzibar kutokana na ongezeko kubwa la  hoteli za Kitalii zilizopo sehemu mbali mbali mijini na Vijijini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Kampuni hiyo kwa uamuzi wake iliyochukuwa  wa kutaka kusaidia miradi mbali mbali ya kilimo hapa Zanzibar.

Aliushauri Uongozi huo kufikiria namna unavyoweza kusaidia miradi hiyo kwa njia ya utaalamu wa umwagiliaji maji mashamba.

Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali asili Zanzibar Nd. Afan Othman Maalim alisema yapo maeneo mengi ya uzalishaji wa mazao ya Mbatata na Vanila hapa Nchini ambayo yanaweza kutumiwa na Kampuni hiyo kwa njia ya Ubia.

Nd. Afan aliyataja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni pamoja na Bambi, Selemu pamoja na Kizimbani.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>