Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi SeIF Ali Iddi akiwa pamoja na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi kwenye chakula maalum cha usiku walichoandaliwa wajumbe wa Bodi Tendaji ya Mfuko wa Kimataifa wa Kilimo { IFAD } hapo Serena Hoteli Shangani Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo { IFAD } Bwana Rasit Pertev akijipatia mlo kwenye dhifa Maalum walioandaliwa wajume wa Bondi ya Mfuko huo hapo Serna Hoteli Shangani.
Mkuu wa Programu ya Mfuko wa IFAD Tanzania Dr. Mwatima Abdulla Juma ,Mkurugenzi wa Mfuko huo Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bwana Perin Saint Ange, pamoja na wajumbe wengine wa bodi ya mfuko huo wakijipatia mlo kwenye dhifa hiyo.
Mkuu wa Bodi Tendaji ya Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo { IFAD } yenye Makao Makuu yake Nchini Italy Dr.Yaya Olaniran akifafanua malengo ya mfuko mara baada ya dhifa maalum ya chakula cha usiku waliyoandaliwa kwenye Hoteli ya Serena Inn Shangani Mjini Zanzibar.Kulia ya Dr. Yaya ni Mkurugenzi wa Mfuko huo Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bwana Perin Saint Ange na kushoto yake ni Katibu Mkuu wa Mfuko huo wa { IFAD } Bwana Rasit Pertev.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Bodi Tendaji ya Mfuko wa Kimataifa wa Kilimo { IFAD } mara baada ya dhifa maalum waliyoandaliwa wageni hao hapo Serena Hoteli Shangani.
Mkurugenzi wa Mfuko wa IFAD Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bwana Perin Saint Angeakitoa shukrani mara baada ya kumalizika kwa dhifa maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya Ujumbe wake.
Balozi Seif akiagana na baadhi ya wajumbe wa Bodi Tendaji ya Mfuko wa IFAD baada ya kukmilika kwa dhifa maalum hapo Hoteli Serena Inn Shangani Mjini Zanzibar.Picha na Hassan Issa wa – OMPR