Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa akizindua wa huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea Jumamosi Mei 7, 2014 wakati wa akizindua wa huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dkt. Joseph Komwihangiro, Mkurugenzi wa Marie Stopes kwa kuwa mstari wa mbele katika huduma na elimu za mzazi wa mpango Jumamosi Mei 7, 2014 wakati akizindua huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo. Wengine toka kushoto ni Mama Salma Kikwete, Mlezi wa MEWATA, Dkt. Serafina Mkuwa, Mwenyekiti wa MEWATA, Mhe. Kebwe Steven Kebwe (Mb.), Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kulia kabisa ni Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Ismail Aden Ragge.
Rais Kikwete akiwasalimia Kinamama waliofika katika uzimnduzi huo na kuchunguza Afya zao.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanakwaya wa kambi ya Msange JKT ya Tabora Jumamosi Mei 7, 2014 baada ya kuzindua huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mbunge wa Tabora Mjini Mhe Ismail Aden Ragge Jumamosi Mei 7, 2014 baada ya kuzindua huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameamuru Jeshi la Polisi kupeleleza na kisha kuwachukulia hatua mara moja watu wote wanaotuhumiwa kwa wizi na ubadhilifu katika vyama vya ushirika mkoani Tabora.
Rais Kikwete amesikitishwa sana na tuhuma hizo zilizosababisha kuwepo kwa tatizo la muda mrefu kwa wakulima wa tumbaku kwa kutokulipwa stahili zao na vyama vya ushirika kwa muda mrefu.
Alisema: "Kwa upande wa tatizo la wakulima wa tumbaku kutokulipwa stahili zao na vyama vya ushirika nimeelezwa na kulielewa. Kuna tuhuma za wizi na ubadhilifu.
“Nimemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi atume watu wake wa upelelezi wa makosa ya Jinai waje wafanye uchunguzi ili wahusika wakamatwe na kufikishwa Mahakamani na kupewa adhabu zinazostahili.
“Ameniahidi kuwa keshokutwa (Jumatatu) watu hao watakuja. Wapeni ushirikiano unaostahili ili tukomeshe uhalifu na dhuluma zinazofanywa na Maofisa wa Vyama vya Ushirika na taasisi za fedha kwa muda mrefu sasa".
Rais aliyasema hayo Jumamosi Mei 7, 2014 wakati akizindua huduma za uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti Mkoani Tabora, katika uwanja wa Chipukizi mkoani humo.
Rais Kikwete alisisitiza kwamba zoezi la kuchukuliwa hatua watuhumiwa wa wizi na ubadhilifu katika vyama vya ushirika lisifanywe la kisiasa, na kwamba asiogopwe wala kuonewa haya mtu yeyote anayehusika hata awe nani.