Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wezi Waiba Mungu wa Mabaniani.

$
0
0
Na Mwandishi wetu
 
POLISI Mkoa wa Mjini Magharibi wanawatafuta watu waliomuiba Mungu wa Mabaniani katika Jamat la Kiponda mjini Zanzibar.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, amethibitisha tukio hilo na kusema wizi huo umefanywa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Alisema wezi hao walimuiba Mungu huyo bila kuvunja mlango wala kufuli za Jamat hilo, hali inayothibitisha kwamba wizi huo umefanywa na miongoni mwa waumini wa Jamat hilo.

“Tunaendelea kuwatafuta wezi wa Mungu huyu lakini uchunguzi wa awali unaonesha wezi hawatoki mbali, lazima wanatoka ndani ya Jamat kwa sababu hakuna mlango wala kufuli zilizovunjwa,” alisema.

Jamat hilo ni maarufu kwa shughuli mbali mbali zinazofanywa na jamii ya Kibaniani.

Aliwataka watu wanaojua taarifa za wizi huo kuwasiliana na polisi ili wahusika watiwe nguvuni.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>