Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji Francis Mutungi, kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita ya Agosti 2, 2013.
Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania, kanda ya Dodoma