Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kiwanda cha Sukari kujengwa Pemba

$
0
0
 Meneja Mkuu wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha sukari Micheweni Pemba Bwana Satish Purandare akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif azma ya Kampuni yake ya kutaka kujenga kiwanda cha sukari Kisiwani Pemba.
 Bwana Satish akimuonyesha michoro ya ujenzi wa kiwanda cha sukari kinachotarajiwa kujengwa katika maeneo huru ya uwekezaji micheweni Pemba baada ya kukamilisha taratibu zote za uwekezaji.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiupongeza Uongozi wa Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Sukari Pemba kwa uamuzi wao waliouchukuwa baada ya kufanikiwa mradi kama huo kwenye kiwanda cha sukari Mahonda.


Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Nd. Julian Raphael, Katibu Mkuu wizara ya Fedha Nd. Khamis Mussa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Nd. Afan Othman Maalim.


Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda unakusudia   kujenga kiwanda chengine cha Sukari Ukanda wa Maeneo huru ya uwekezaji Vitega Uchumi yaliyopo Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika azma yake wa kuwekeza miradi ya Kiuchumi hapa Zanzibar.
 
Uamuzi wa kuanzisha mradi huo mpya umekuja kufuatia mafanikio makubwa yaliyopatilana mara baada ya kuanza rasmi kwa uzalishaji wa Sukari katika Kiwanda cha Mahonda kiliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 
Meneja Mkuu wa Mradi huo wa Kiwanda cha Sukari Pemba { Pemba Talon Sugar Factory ltd – PTSFL }  Bwana Satish Purandare alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Vuga Mjini Zanzibar.
 
Bwana Satish alisema Uongozi wa Mradi huo unakusudia kuanza kutoa elimu kwa Wananchi wa Maneo ya Kiuyu, Micheweni pamoja na Wete wale watakaoamuwa kujishughulisha na ukulima wa Miwa ili baadaye wapate fursa ya kukiuzia miwa yao Kiwanda hicho ili kiendeshe uzalishaji wa Sukari.
 
Alisema kazi ya uzalishaji wa miwa itakuwa ikiendeshwa na wananchi watakaokizunguuka kiwanda hicho ili kutoa fursa ya ajira itakayowawezesha kujipatia kipato na kupunguza umaskini.
 
Mkurugenzi Mkuu huyo wa PTSFL alimueleza Makamu wa mPili wa Rais wa Zanzibar kwamba harakati za ujenzi zinatarajiwa kuanza rasmi mapema mwaka ujao baada ya kukamilika kwa taratibu zote za uwekezaji.



“ Tumepanga kuanza shughuli za ujenzi wa Kiwancha hicho cha Sukari katika eneo huru la uwekezaji vitega uchumi liliopo Micheweni  mwakani ambapo matarajio yetu ni kuanza  kuzalisha sukari mwezi Oktoba mwaka     2015 “. Alifafanua Bwana Satish.
 
Alifahamisha kwamba Kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha sukari  Tani 1200 kwa kiwango cha  ekari 300 watakazolima wakulima na wananchi hao ikiwa ni hatua ya awali ya kuanza kwa mradi huo.
 
Bwana Satish alieleza kwamba mrdi huo unatarajiwa kugharimu zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni { U$ 15,000,000 } kwa ujenzi wa Kiwanda na Doma Milioni Tano zitahusika katika uzalishaji wa mashamba utaosimamiwa na Wakulima binafsi.
 
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushukuru Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kwa hatua iliyofikia ya kuanza kwa uzalishaji wa Sukari.
 
Balozi Seif alisema hatua hiyo ambayo inafaa kupongezwa ni matunda mazuri yanayoanza kuchomoza ambayo mbali ya kuongeza mapato ya Taifa lakini pia yamesaidia kutoa ajira kwa baadhi ya wananchi hapa Nchini.
 
“ Mradi wenu mnaotaka kuutekeleza Micheweni Pemba  ni matunda mazuri ya mradi  mliouanzisha  awali wa uzalishaji wa sukari katika kiwanda cha Mahonda ambao tayari umeanza kutoa faida “. Alisema Balozi Seif.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kwamba ongezeko  la ujenzi wa viwanda vya sukari kwa kiasi Fulani litasaidia kupunguza mfumko wa bei ya bidhaa hiyo kiholela hapa Nchini.
 
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikutana kwa mazungumzo na Rais wa chuo Kikuu cha Franklin  Columbus kilichopo Jimbo la Ohio Nchini Marekani Dr. Godfrey Mendes.
 
Katika mazungunzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Vuga Mjini Zanzibar Dr. Godfrey Mendes alimuelezea Balozi Seif azma ya Chuo Kikuu hicho ya kutaka kujenga Kampas yake hapa Zanzibar.
 
Dr. Mendes alisema Franklin University Columbus, Ohio USA imekuwa ikitoa huduma za elimu ya juu ya vyuo vikuu katika masomo ya Sayansi, Kompyuta, Ustawi wa Jamii katika Mataifa 12 Duniani.
 
Alifahamisha kwamba Uongozi wa Chuo hicho umeridhika na hali ya mazingira na utulivu wa Zanzibar na kufikia azma ya kutaka kuanzisha kampas ya chuo hicho hapa Zanzibar itakayoshirikisha wanafunzi kutoka nchi mbali mbali Duniani.
 
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inaendelea kukaribisha wawekezaji wa sekta mbali mbali za kiuchumi, ustawi wa Jamii na zaidi masuala ya elimu.
 
Katika kujiimarisha kuzalisha wataalamu wazalendo NCHINI Balozi Seif alisema Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZA } kinaendelea na mikakati ya kufundisha mafunzo ya Udaktari sambamba na fani ya kilimo ili kuondosha upungufu wa wataalamu katika fani hizo mbili muhimu kwa ustawi wa Taifa.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuomba Uongozi wa Chuo hicho Kikuu cha Franklin Columbus Ohio cha Nchini Marekani kuwasiliana na Uongozi wa chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZA } katika kutafuta mbinu za kufanikisha mipango hiyo.
 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>