Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Zanzibar yajipanga kutokomeza maradhi ya kichocho

$
0
0
 Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dkt. Sira Ubwa Mamboya akifungua Mkutano wa kufanya tathmini mafanikio ya changamoto za mradi wa miaka mitano wa kutokomeza maradhi ya Kichocho Zanzibar (kushoto) Prof. David Rollinson Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya wanyama, na (kulia) Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Afya Juma Rajab
 Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa kutathmini mafanikio ya changamoto za mradi wa miaka mitano wa kutokomeza maradhi ya Kichocho Zanzibar uliofanyika Juni 17 katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
 Prof. David Rollinson Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya wanyama na, akielezea hatari za ugonjwa wa Kichocho na athari zake katika Mkutano huo.
Mgeni rasmin Naibu Waziri wa Afya Zanzinzibar Dkt. Sira Ubwa Mamboya katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano huo, huko Zanzibar Ocean View Hotel Mjini Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga- Maelezo ZNZ).
 
NGUVU za pamoja kati ya Wizara ya Afya Zanzibar, Nchi Washirika wa Maendeleo na Taasisi ya SCORE yenye makao makuu yake jijini Georgia Marekani, zimesaidia kupunguza kasi ya maradhi ya kichocho Unguja na Pemba.
 
Aidha mafanikio hayo yameelezewa kuwa yametokana na mkakati madhubuti uliowekwa na wizara hiyo kuhakikisha inatokomeza kabisa maradhi hayo yanayowaathiri kwa kiasi kikubwa watoto wenye umri kati ya miaka 7 na 14.
 
Akifungua mkutano wa kufanyia tathmini mafanikio ya changamoto za mradi wa miaka mitano wa kutokomeza maradhi hayo nchini Zanzibar huko hoteli ya Zanzibar Ocean View, Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya, amesema ufanisi huo usingepatikana bila ya ushirikiano kati ya pande hizo.


Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya Juma Duni Haji, Dk. Sira amesema mpango huo ulihitaji nyenzo za kitaalamu na fedha nyingi, ambazo Serikali ya Zanzibar isingeweza kumudu kwa wakati muafaka bila kushirikisha wadau mbalimbali wa kimataifa.
 
Amesema chini ya uongozi wa Profesa Dan Colley wa Chuo Kikuu cha Georgia, utafiti ulifanyika kwa mafanikio ili kubaini ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa kichocho nchini.
Mapema akiwasilisha ripoti ya utafiti wa Kitengo cha
 
Maradhi Yasiyopewa Kipaumbele Dk. Khalfan Mohammed, amesema kwa sasa mradi huo wa miaka mitano ambao umetimiza miaka miwili, unahusisha shehia 90 (Pemba 45, Unguja 45).
 
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO
 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>