Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mali kachara kudhibitiwa

$
0
0
Na Mwanajuma Mmanga
IDARA ya mazingira Zanzibar ipo mbioni kuandaa sheria ya kuwadhibiti wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa chakavu  kutoka nje.

Sheria hiyo inakuja baada ya kuonekana Zanzibarkuwa jaa la bidhaa chakavu kutoka ng’ambo ambazo huingizwa na wafanyabiashara au Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi.

Mkurugenzi wa idara hiyo,Sheha Mjaja Juma, aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofsini kwake Maruhubi.

Alisema Zanzibar sasa imekuwa jaa la bidhaa chakavu hali inayohatarisha mazingira na afya za wananchi.
Aidha alisema wakati mwingi bidhaa hizo huja sambamba na mende wengi wadogo, ambao wanasababisha athari kubwa katika makazi ya watu.


Alisema sheria hiyo iutasaidia kupunguza uingizaji wa bidhaa nyingi zisizokuwa na viwango.


Alitoa wito kwa wafanyabiashara kuingiza bidhaa zenye viwango badala ya kuingiza bidhaa chakavu kwa sababu tu wanazipata kwa bei rahisi au bure. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>