Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Magharibi Bi. Raisa Abdallah baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya hiyo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwapungua mkono wananchi katika eneo la Saateni wakati akiendelea na ziara yake ya kuwatembelea wagonjwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimfariji kijana Hamza Omar Juma, anayesumbuliwa na matatizo ya moyo katika eneo la Mtoni Kidatu.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwapungua mkono wananchi, wakati akiendelea na ziara yake ya kuwatembelea wagonjwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika mitaa ya Muembe Makumbi kuendelea na ziara yake ya kuwatembelea wagonjwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi. (Picha na Salmin Said, OMKR).
Na Hassan Hamad OMKR
Wagonjwa wapatao 35 walioko majumbani wamepatiwa huduma na ushauri wa kiafya katika Wilaya sita za Unguja.
Hatua hiyo imefikiwa kufuatia ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar mjini na vijijini.
Katika ziara hiyo, pamoja na mambo mengine wagonjwa wamekuwa wakipatiwa baadhi ya dawa muhimu kulingana na maradhi yanayowakabili, sambamba na kupatiwa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na matatizo yao.
Mhe. Maalim Seif amekamilisha ziara yake ya siku tatu ya kutembelea wagonjwa kwa upande wa Unguja iliyoanzia Mkoa wa Kaskazini Unguja na kumalizikia Mkoa wa Mjini Magharibi.
Makamu wa Kwanza wa Rais anatarajiwa kufanya ziara kama hiyo katika Mikoa miwili ya Pemba kuanzia wiki ijayo.