Na Mwanajuma Mmanga.
WAKATI mwezi mtukufu wa Ramadhani ukiendelea wakulima wa vijiji vya Donge Vijibweni na Donge pwani,wamelalamikia tabia ya wizi wa mazao iliyoshamiri, kitendo kinachowarejesha nyuma wakulima.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wanavijiji hao walisema mazao kama muhogo, ndizi, viazi, mananasi,miwa na mapapai na mbegu za mihogo ndiyo yanayoibiwa kwa wingi.
Walisema mara nyingi mazao hayo kuibiwa nyakati za usiku wakati wakulima tayari wakiwa wameshaondoka.
Walisema kutokuwepo polisi jamii ndiko kulikosababisha ongezeko la wizi huo.
Naye sheha wa shehia ya Donge vijibweni, Abdalla Abrahman Machano, alikiri kuwepo kwa matukio hayo na kusema vijana wa mitaani ndio wanaoshiriki wizi huo.
Aliwashauri wakulima kushirikiana ili kuhakikisha wanakabiliwa na wizi huo pamoja na mifugo inayoharibu mazao yao.