Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Washtakiwa kesi ya mauaji ya watu 229 huru · Ni ya Mv. Spice Islander

$
0
0
Na Khamis Amani
Mahakama Kuu Zanzibar,imewaachia huru washtakiwa 12 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya  ya mauaji ya bila kukusudia ya watu 229, katika ajali ya meli ya Mv Spice Islanders 1.

Miongoni mwa washtakiwa hao alikuwemo Mwakilishi wa jimbo la Muyuni, Jaku Hashim Ayoub.
Uamuzi wa kuachiliwa huru washitakiwa hao,ulitolewa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, baada ya kesi hiyo kushindwa kusikilizwa kwa kipindi kirefu.

Hata hivyo, hukumu hiyo imepingwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na amepanga kukata rufaa mahakama ya rufaa Tanzania.

Wakili wa serikali Omar Khalfani Sururu, alidai hakuridhika na uamuzi huo na kuamua kuwasilisha  notisi ya kukata rufaa.

Tayari DPP ameshawasilisha notisi ya kukata rufaa na matayarisho ya mwenendo wa kesi hiyo yanaendelea, ili waweze kuanza kazi ya kuwasiliosha rufaa yao mahakama ya juu.

Katika hukumu yake Jaji Mkuu alisema kesi hiyo imeshindwa kusikilizwa kwa muda mrefu na kusababisha usumbufu kwa washitakiwa.

Kabla ya kuondolewa mahakamani kesi hiyo ambayo upelelezi wake ulikuwa tayari umeshakamilika,ilifikishwa katika kikao kilichopita kwa ajili ya kusikilizwa, lakini upande wa mashitaka ulitaka kuwasilisha mahakamani orodha ya maelezo ya mashahidi wa ziada.


Hata hivyo,jopo la Mawakili wa utetezi ulioongozwa na Masumbuko Lamwai, ulikataa hatua hiyo ya upande wa mashitaka na kudai haikubaliki kisheria kwa kuzingatia kesi hiyo ipo katika hatua za usikilizwaji.

Walidai upande wa mashitaka umekuwa ni kikwazo cha usikilizwaji wa kesi hiyo iliyodumu mahakamani hapo kwa zaidi ya miaka miwili na kuiomba mahakama kuiondosha kutokana na upande huo kukosa jipya la kuiambia mahakama.

Walidai kitendo cha kuongezwa orodha ya maelezo ya mashahidi katika kesi ya usikilizwaji haikubaliki, hoja ambazo ziliungwa mkono na Jaji Mkuu na kuamua kuwaachilia huru washitakiwa hao.

Kesi hiyo ilikuwa bado haijasikilizwa kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 209 cha sheria za mwenendo wa jinai (CPA) nambari 7/2004 sheria za Zanzibar.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, shitaka lotelote lenye dhamana linapaswa kusikilizwa ndani ya kipindi cha miezi minne, endapo halikusikilizwa mahakama imepewa uwezo wa kuiondosha mahakamani.

Mbali ya Jaku, washtakiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa Said Abdallah Kinyanyite aliyekuwa nahodha wa meli hiyo anaedaiwa kufa maji siku ya tukio hilo, Abdallah Mohammed Ali pamoja na Yussuf Suleiman Issa (Kassu).

Wengine ni Simai Nyange Simai, Haji Vuai Ussi, Abdallah Mohammed Abdallah, Juma Seif Juma, Hassan Mussa Mwinyi, Salim Said Mohammed Battashy, Makame Hasnuu Makame pamoja na Shaibu Said Mohammed Battashy.

Wote hao walidaiwa kwamba, kutokana na dhamana na majukumu yao waliyonayo juu ya usalama wa abiria, mizigo na meli hiyo ya MV Spice Islander I, kwa uzembe walishindwa kutekeleza majukumu yao na kuiachia meli hiyo kuchukua abiria na mizigo zaidi ya uwezo wake.

Ilidaiwa washtakiwa hao hawakujali usalama na kusababisha meli hiyo kushindwa kuendelea na safari ya Pemba ikitokea Unguja na hatimae kuzama katika eneo la mkondo wa Nungwi na kusababisha vifo vya abiria 229 waliokuwemo ndani yake.

Meli hiyo ilidaiwa kuzama Septemba 9, 2012 ilipokuwa ikitokea bandari ya Malindi mjini Unguja kuelekea kisiwani Pemba, kitendo ambacho kilielezwa ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 195 cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.


Awali washitakiwa wote hao walikana mashitaka yao waliposomewa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo na hadi wanaachiliwa huru walikuwa nje kwa dhamana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>