KATIKA Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC, John Mkawawa, akizungumza na waandishi wa habari kisiwani Pemba, juu ya uimarishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknologia mpya ya ‘BVR’ kutoka ile ya zamani ya OMR, mkutano huo ulifanyika hoteli ya hifadhi Chakechake Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)
AFISA kutoka wizara ya ardhi, makaazi, maji na nishati Pemba bw Salim, akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya kuzielewa sheria za ardhi kwa wasaidizi wa sheria wa majimbo ya Pemba, mafunzo yalioandaliwa na ‘ZLSC’ na kufanyika afisini kwao mjini Chakechake Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)
MWANAHARAKATI wa asasi za kiraia Pemba, Juma Bakari Alawi ‘JB’ akiwafahamisha wanajumuia ya mendeleo ya wanawake wa kijiji cha Tundauwa ‘JUMATU’ wilaya ya Chakechake, namna ya kujaza fomu za tathimini, baada ya kumaliza mradi wa haki za binaadamu na utawala bora, mkutano huo ulifanyika skuli ya Kilindi (picha na Haji Nassor,Pemba)
WANAFUNZI wa chuo cha elimu na biasahara Zanzibar ‘ZCBE’ wakiwa darasani kuanza mwana mpya wa masomo, ambao umezunduliwa juzi na mkuu wa chuo hicho Abdull-wahabi Said Bakari, hafla iliofanyika chuoni hapo Vitongoji wilaya ya Chakechake Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)
MUKUU wa Idara ya Ustawi wa Jamii kutoka wizara ya uwezeshaji, ustawi wa Jamii, vijana wanawake na watoto Abduu Salim Mohamed, akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa madawati ya watoto, vituo vya huduma vya mkono kwa mkono na askari wapelelezi, mafunzo yalioandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar ‘ZLSC’, yaliofanyika hoteli ya hifadhi Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)
PICHA ya pamoja baina ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa madawati ya watoto, vituo vya huduma vya mkono kwa mkono na askari wapelelezi, mafunzo yalioandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC, yaliofanyika hoteli ya hifadhi Pemba, mara baada ya kufugnguliwa mafunzo hayo ya siku mbili (picha na Haji Nassor, Pemba)
AFISA mipango wa kituo huduma za sheria Zanzibar ZLSC, Khalifan Amour, akiwasilisha mada ya sheria ya mtoto no 6, ya mwaka 2011, mbele ya washiriki ambao ni watendaji wa madawati, vituo vya mkono kwa mkono na askari wapelelezi, kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo, yaliofanyika mjini Chakechake (picha na Haji Nassor, Pemba)