Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wanaume 120,000,Wafanyiwa Tohara

$
0
0
Na Kadama Malunde, Simiyu
ZAIDI ya wanaume 100,000 katika wilaya ya Baridi mkoani Simiyu, wanatarajiwa kutahiriwa ndani ya kipindi cha miaka mitano katika mradi wa tohara kwa wanaume wilayani humo ulio chini ya shirika lisilo la kiserikali Intra Health kwa kushirikiana na serikali.

Mradi huo unalenga kuwafikia wanaume 127,840, kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo watakaohusika ni watoto kuanzia miaka 10 hadi 30.

Hayo yalibainishwa juzi na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Asey John katika ufunguzi wa kituo cha kutolea huduma hiyo katika hospitali ya wilaya, ufunguzi uliofanya na Mwenge wa uhuru.

Alisema mradi huo ulianza mwaka 2010 ambapo mpaka sasa una mika mitatu tangu uanzishwe na unatarajiwa kufikia mwisho mwaka 2015.

Alibainisha kuwa tangu kuazishwa kwa mradi huo jumla ya wanaume 27,969 kutoka mwaka 2010 hadi Julai mwaka huu 2013 wamefanyia tohara, huku akibainisha changamoto mbalimbali ambazo wamekutana nazo ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa elimu kwa wanaume juu ya umuhimu wa tohara.

Aliongeza changamoto nyingine ni kuwepo kwa imani potofu kwa baadhi ya wanaume kwamba kufanya tohara kunasababisha ugumba.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Juma Ali Simai aliwataka wanaume kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo, sambamba na kuwataka kuachana na imani hizo potofu, huku akiwasisitiza wanawake kuwashawishi waume zao kwenda kupata huduma hiyo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>