Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

UKAWA wameguka .Kamati ya Shamsi yashindwa kupata theluthi mbili

$
0
0
Na Mwantanga Ame,Dodoma
Kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), inazidi kubomoka, baada ya wajumbe wengine kutoka vyama vya CHADEMA na CUF kuonekana katika viwanja vya bunge.

Tayari wajumbe kutoka kundi la UKAWA walioonekana katika viunga vya bunge wamefikia sita.

Hata hivyo, viongozi wakuu wanaounda umoja huo wanaendelea na msimamo wa kutorudi bungeni.
UKAWA, waliamua utoka bungeni Aprili mwaka huu, wakilalamikia kubaguliwa na kudhalilishwa.

Hali hiyo, ilisababisha viongozi mbali wakiwemo wa kisiasa na dini kuwaomba kurejea bungeni kuendelea kujadili rasimu.

Jana asubuhi mwandishi wa habari hizi, aliwashuhudia wajumbe wengine kutoka chama cha CUF wakifanya usajili.

Waliojitokeza jana ni Mbunge wa Mtanda mjini, Said Arif (CHADEMA), huku pia kukiwa na wajumbe wengine watano kutoka UKAWA waliojisajili na kupokea posho wakiwemo kutoka CUF.


Katibu wa bunge hilo, Yahya Khamis Hamad, alithibitisha kuwepo kwa wajumbe hao na kusema hadi jana asubuhi walishafikia sita huku kukiwa na taarifa za Mbunge mwengine kujisajili.

Alisema hadi mchana wabunge wote waliosajiliwa walikuwa 425 wakiwemo sita kutoka UKAWA.

Aliiwataja wajumbe hao kuwa ni Clara Mwaitupa Mbunge wa Viti Maalum (CUF),Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (CHADEMA), Mbunge wa Maswa, John Shibuda, Ali Omar, Jamila Abeid na Fatma Mohammed Hassan.

Alisema baadhi ya wajumbe hao wameanza kupokea posho ya shilingi 230,000 na shilingi 70,000 huku wengine wakiwa bado jawajalipwa kutokana na  kubanwa na kanuni.

Alisema utaratibu uliotolewa ni kwamba mjumbe anatakiwa kupewa posho ya siku saba kwa ajili ya kujiweka vizuri.

Wajumbe wa bungehilo tayari wameanza mjadala kwenye kamati 12, ambazo zinajadili sura 15 za rasimu hiyo, kazi ambayo itakamilika Oktoba.

Taarifa za ndani ambazo Zanzibar Leo imezipata nje ya bunge, huenda idadi ya wajumbe hao ikaongezeka wiki ijayo baada ya UKAWA, kumaliza mjadala wao unaotarajiwa kufanyika mjini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati namba mbili ya bunge, Shamsi Vuai Nahodha, amesema baadhi ya sura ya rasimu ya katiba zimekumbwa na msukosuko na kutopata theluthi mbili na sasa watasubiri kura kuu ya bunge.

Nahodha, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa jengo la hazina mjini hapa.

Alisema katika mjadala wao ibara ya 19 na 22 za rasimu hiyo, zilikosa kupata maamuzi baada ya kutopigiwa kura kutokana na kutotimia kwa akidi ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema kwa mujibu wa sheria,ibara hizo zlitakiwa kupata theluthi mbili ya kura kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema wajumbe waliotarajiwa kupiga kura hiyo kwenye kipengele hicho kwa upande wa Zanzibar walitakiwa kuwa 12, lakini alikosekana mtu mmoja, huku sura ya 11 ilikosa mtu mmoja kwa upande wa Tanzania Bara baada ya waliokuwepo kufikia 22 badala ya 23.

Alisema sura hizo zinahusu maadili ya uongozi na utumishi wa umma, ambayo imebeba vipengele vinavyohusu dhamana ya uongozi wa umma na kanuni za uongozi wa umma pamoja na zawadi katika utumishi wa umma.

Alisema kuanzia sasa kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, zawadi hiyo itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ataiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kupitia Katibu Mkuu wa Wizara au kiongozi wa taasisi ya serikali inayohusika.

Alisema bunge hilo litatunga sheria itakayosimamia pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano.

Aidha alisema hadi jana hakukuwa na mvutano wowote uliojitokeza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>