Na Joseph Ngilisho,Arusha
MKWARE wa ngono jijini Arusha, (jina linahifadhiwa) maarufu Boyoo(22) mkazi wa Sombetini, amenusurika kipigo baada ya kubambwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 15 anayesoma kidato cha tatu, skuli ya sekondari ya Peace House.
Mtuhumiwa alikuwa amemuweka kinyuma mwanafunzi huyo,huku wazazi wake wakiamini yupo masomoni.
Boyoo ambaye anamiliki studio ya kudurufu kazi za wasanii ,anadaiwa amekuwa na tabia ya kufanya ngono na vitoto vidogo na kuwabadilisha kama nguo kwenye ‘geto’ lake.
Sekeseke la kubambwa kwa kijana huyo lilitokea jana majira ya asubuhi baada ya wazazi wa mwanafunzi huyo kupata taarifa kuwa mtoto wao amewekwa kinyumba katika ‘geto’ la mtuhumiwa kwa muda wa wiki moja huku familia yake ikiamini kwamba tayari yupo skuli akiendelea na masomo yake.
Wazazi wa mwanafunzi huyo ambao ni wakazi wa eneo la Unga Limitedi jijini hapa,walifika katika ‘geto’ hilo na baada ya kugonga mlango , ndipo walipokutana uso kwa uso na mtoto wao akiwa na kanga moja.
“Sisi tulijua mtoto yupo skuli lakini tuliopata taarifa kuwa hayupo skuli na ndipo tulipofuatilia dereva bodaboda aliyempakia siku hiyo na tulipomhoji vizuri huku tukimtishia kumpeleka polisi, alielekeza mahala mtoto alipo na tulipokwenda tulimkuta,” alisema.
Baada ya mwanafunzi huyo b kukutana uso kwa uso na wazazi wake,alianguka chini na kupoteza fahamu na alizinduka majira ya mchana akiwa hospitali ya mkoa Mount Meru alikokimbizwa kwa matibabu.
Mwanafunzi huyo alikacha masomo tangu Julai 28 mwaka huu na kuhamia kwa mtuhumiwa huyo huku akishindia chipsi na soda na kusahau kwamba wazazi wake wamelipa ada ya shilingi 800,000 kwa ajili ya kumsomesha.
Akizungumza huku akilia, mama mzazi wa msichana huyo,Anna Martini,alisema mtoto wao alitoweka nyumbani siku ya Jmatatu Julai 28,baada ya wazazi wake kumfungashia wakiamini anaenda skuli.
Alisema walipata taarifa kutoka uongozi wa skuli hiyo kuwa mtoto wao hayupo na ndipo walipoanza kumsaka maeneo mbalimbali na kutoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi cha Unga Limited.
Hatua zaidi zilichukuliwa kwa mtuhumiwa huyo kupigwa pingu baada kukamatwa kutokana na wazazi kutoa taarifa polisi.
Hata hivyo, wazazi wa mhuhumiwa walitaka kulimaliza suala hilo ili mtoto wao asifikishwe mahakamani kwa kufanya maelewano ya kuwapatia fedha baadhi ya askari polisi.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha, hakupatikana kuzungumzia suala hilo baada ya simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.
Mwanafunzi huyo aliamuriwa kwenda kupimwa ujauzito pamoja na maambukizi ya magonjwa ya kujamiiana.