Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

ACT chataka mjadala katiba mpya usitishwe

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
CHAMA cha Alliance for Chage and Transparence-Tanzania (ACT) kimemuomba Rais Jakaya Kikwete kulivunja bunge la katiba kwa kile kinachodai limekosa  uhalali wa kisiasa.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba, wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alisema ACT Tanzania kinasikitishwa na  bunge maalum kuendelea kujadili katiba ilihali kundi kubwa la wajumbe wako nje ya mchakato.

Alisema kama wabunge wa upande mmoja wataruhusiwa kujadili katiba, Watanzania wasitarajie kupata katiba waitakayo na kwamba haitakuwa na tofauti na katiba ya sasa.


Aidha,chama hicho kimesekitisha na na viongozi wa vyama vya siasa wa CCM na vile vinavyounda kundi la UKAWA kwa kushindwa kupata muhafaka kuhusu muundo wa muungano.

Alisema ni aibu kushuhudia wanasiasa wakiteka mchakato wa katiba na kujadili maoni ya vyama vyao badala ya maoni ya wananchi ambao ndio wamiliki wa katiba.

Aidha chama hicho kimetoa mapendekezo kadhaa ikiwemo kuruhusiwa mgombea binafsi,kushusha umri wa mgombea wa urais ili kuwapa fursa vijana kugombea nafasi hiyo.


Kimewaomba Watanzania wote kuungana kushinikiza mchakato wa katiba usimamishwe.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>