Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wananchi Mkoa wa Kusini watakiwa kuwa na ushirikiano kwa lengo la kulinda Usalama

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Bw. Ahmed Shehe, akizungumza katika Mkuta wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kusini Unguja, Manahodha na wamiliki wa vyombo vidogo vya usafiri baharini katika Ukumbi wa SUZA Tunguu. (kuli) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Idrissa Muslim Hija na (kusho) Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri Baharini Bi. Sheikha A. Mohammed.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Idrissa Muslim Hija akifungua Mkutano wa siku moja wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kusini pamoja na masheha, manahodha na wamiliki wa vyombo vidogo vya usafiri baharini uliandaliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini huko Tunguu.
 Mwanasheria wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Nd. Rashid J. Mohammed akiwasilisha mada kuhusu sheria za usafiri wa baharini
 Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo
 Kamanda wa KMKM Kamandi ya Kusini Unguja CDR. Moh’d Mussa (Mkobani) akitoa mchango katika Mkutano huo.
Sheha wa Unguja Ukuu Tindini Mzee Jecha Ali akitoa mchango wake katika Mkutano huo. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).
Na Miza Othman Makame  Maelezo
       
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Idrissa Muslim Hija amewataka wananchi wanaotumia  Bandari za Mkoa wa Kusini kuwa na Umoja na Ushirikiano kwa lengo la kulinda  usalama ndani ya  Mkoa huo.
 
Ameyaeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na wakuu wa kamati za ulinzi na usalama,  Masheha, Manahodha na wamiliki wa vyombo vidogo vidogo vya  usafiri wa baharini pamoja na wananchi wa Mkoa huo katika  Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibnar (SUZA)  Tunguu.
 
Amesema  Masheha  wanajukumu kubwa katika kulinda na  kusimamia  usalama wa bandari zote zilizomo ndani ya Mkoa huo ili kuhakikisha sheria zilizowekwa zinafuatwa.
 
“Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA) imeundwa kusimamia Manahodha wa vyombo vya Baharini na kila mmoja anahaki ya kulinda na kuzuia uhalifu usiweze kutokea”, alisema Idrisa Muslim Hija.
 
Mkurugenzi wa usajili na vyeti Sheikha Juma amesema  sheria za kulinda usalama wa bandari  zimeshaanzishwa tangu mwaka 2010 kwa hivyo kila raiya  analazimika kuzifuate ili kuondosha migogoro isiyo ya lazima.
 
 Amesema hadi hivi sasa wameshaanza kusajili vyombo vidogo vidogo vyenye urefu wa ziraa  nane au urefu wa mita nne kwani kufanya hivyo kutapelekea kurahisisha upatikanaji  wa chombo cha muhusika wakati anapotokewa na tatizo ikiwemo kupotea, kuungua na hata kuibiwa kwa chombo chenyewe.
 
“Nilazima raiya atekeleze  sheria zilizopo ili kujiepusha  na majanga na panapotokea ajali  muhusika aweze kulipwa fidia”, alisema Sheikha Juma Mohammed.
 
Aidha amesema ni lazima Manahodha wawe mstari wa mbele  kutekeleza
 sheria za bandari zilizopo  kwa lengo la kusaidia Serikali kuipatia mapato ili iweze kujiimarisha kiuchumi.
 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles