Mahakama kuu Zanzibar leo imesikiliza ombi la dhamana lililowasilishwa na Mawakili wanaomtetea aliewahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mh.Mansour Yussuf Himid.
Baada ya kusikiliza hoja za kisheria kutoka pande zote mbili za mawakili Mahakamani hapo, Jaji Abraham Mwampashi amesema Mahakama kuu haina pingamizi la kupokea ombi la Dhamana kwa Mansour kwa sababu limezingatia vigezo vyote vya kisheria.
Hivyo Jaji Mwampashi amepeleka mbele ombi hilo hadi tarehe 18 mwezi huu kwa ajili ya kutolewa maamuzi ya dhamana yake ambapo pia siku hio ndio siku iliopangwa kwa ajili ya kusikilizwa kesi inayomkabili Mh. Mansour .
Mahakama kuu Vuga imeamuru kurudishwa tena rumande kwa Mansour hadi tarehe 18 mwezi huu ambapo maamuzi juu ya maombi ya dhamana yake yatakapotolewa pamoja na kusikilizwa kwa kesi yake ya msingi inayomkabili.
Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 3/8/2014 majira ya asubuhi, Jeshi la Polisi Zanzbar kitengo cha upepelezi kilifika nyumbani kwa Mansour huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na kufanya upekuzi hatimae kukutwa na silaha kinyume na Sheria.
Credit : Hamed Mazrui via Facebook