Na Abdi Suleiman, PEMBA
WANANCHI kisiwani Pemba, wametakiwa kujenga misingi ya kuwafahamu watu wenye ulemavu na kujuwa mbinu mbali mbali za kuishi na watu hao.
Wito huo umetolewa na washiriki wa Mkutano wa wadau wa kutoafursa kwa watu wasioona, uliondaliwa na Jumuiya ya ZANAB Pemba .
Washiriki hao walisema kuwa, kama jamii ingejenga misingi ya kuwafahamu wenye ulemavu, jinsi gani wanapaswa kuishi nao pamoja matatizo yote hayo yanayowakumba yasingetokeoa.
Mmoja kati ya washiriki hao, Nassor Hafidh kutoka Jumuiya ya Maimamu, alisema kuwa walemavu wa akili wamekuwa wakidhalilishwa kutokana na ulemavu wao.
Alisema kuwa walemavu wasioona wana afadhali katika matukio ya udhalilishaji kuliko walemavu wa akili, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya watu wenye ulemavu.
“Tatizo la yote hao ni ukosefu wa taaluma kwa jamii, jamii iliyo kubwa inaonekana haina elimu, jinsi gani waishi na watu wenye ulemavu”alisema.
Yussuf Hamad kutoka kitengo cha askari wa usalama wa barabarani Mkoani, alisema kuwa Serikali inapaswa kuwashirikisha watu wenye ulemavui kwa kila kitu, sio kuamua jambo bila ya kuwashirikisha hali inayopelekea kuwepo kwa usumbufu baadae.
Alifahamisha kuwa, watu wenye ulemavu wanapaswa kuwekwa karibu katika nafasi mbali mbali za ajira kama ilivyo watu wasio na ulemavu.
“Ajira nyingi zinatolewa ingewekwa angalau alisimia 15% nao wanaajiria, lanini hilo halipo hata ukiangalia majimba yanayojegwa hayako rafiki nao pia”alisema.
Ramadhan Khamis alisema kuwa, kuwepo kwa sheria ya walemavu Zanzibar ni moja ya taua moja mbele, hali ambayo ingekuwa ni nafuu kwao.
Aliyomba serikali kuwapatia walemavu wa sio mashine za nukta nundu, ambayo itaweza kuwasaidia katika masomo yao , kwani walemavu wasioona wamekuwa wakipata tabu wakati wanapohitaji kusoma.
“Utamuona kiongozi anamiliki gari la Milioni 30, lakini kumsaidia mlemavu braina moja ni tatizo kubwa kwakwe, tuwaone hawa ni vijana wetu”alisema.
Kwa upande wake Sabra Nassor kutoka ZANAB Pemba, alisema kuwa suala la elimu mjumuisho kwa walemavu wasiona ni tatizo kubwa sana kwao.
Sabra alisema kuwa, wanafunzi wenye ulemavu wa kutokuona ip[o haja ya kuwekwa pamoja katika skuli zenye bodingi, ili kuweza kusaidiana wakati wa masomo.
Akiwasilisha mada katika mkutano huo, mratib wa Jumuiya ya watu wenye ulamavu wa akili Pemba , Ali Haji Mwadini alisema kuwa, tatizo la kubakwa watu wenye ulemavu bado linaendelea kutendeka kutokana na ulemavu wao.
Alifahamisha kuwa, laiti kama wabakaji hao wangekuwa wakitiwa hatiani basi matendo hayo ya kubakwa na kudhalilisha kwa walemavu lingepungua.
Mratib huyo alisema kuwa, kwa sasa watendaji wa vyombo vya sheria wanapaswa kukubaliana na ushahidi unaotolewa na walemavu mahakamani pale wanapofanyiwa udhalilishaji.
Alifahamisha kuwa, sasa wakati umefika kwa serikali kujenga majengo yatakayofuata suala la mujumuisho wa watu wote, kwani majengo mengi yamekuwa ni kikwazo kikubwa wa walemavu wasioona na hata wengine.