Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Serikali yaanza kuchukua hatua kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Vuga kuhusu Ugonjwa wa Ebola na mikakati ambayo SMZ inaendelea kuichukuwa ili kukabiliana na ugonjwa huo hatari, hadi sasa hakuna mgonjwa alieyegundulikana na ugonjwa huo Zanzibar.
 Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Waziri Mohammed Aboud alipokuwa akitoa tarifa juu ya ugonjwa hatari wa Ebola Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed akifafanua kitu wakati wa Mkuta wake na wanahari.

 Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.

Na Jamila Abdalla , Maelezo

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  imeanza kuchukua hatua mbali mbali za kukabiliana na Ugonjwa hatari wa Ebola ambao unazidi kusambaa katika nchi mbali mbali Barani Afrika.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar kuhusiana na mikakati ambayo SMZ inaichukua ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Waziri Aboud amesema licha ya kwamba Zanzibar hakuna Mgonjwa aliyegundulika kuwa na Ebola lakini mazingira yanaonesha kuwa Zanzibar inaweza kupata maradhi hayo kutokana na kuwa na muingiliano mkubwa na nchi nyingine ambazo tayari zimethiriwa na Ugonjwa huo.


Ametaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari juu ya maradhi ya Ebola na namna ya kujikinga.

 Mh: Aboud amesema kuwa pia serikali itaimarisha taratibu za ugunduzi ,ukaguzina ufuatiliaji wa washukiwa wa ugonjwa huu katika bandari ,viwanja vya ndege,vituo vya afya na jamii kiujumla.

Akiendelea kufahamisha mikakati hiyo waziri huyo amesema kuwa Pia serikali imeandaa maeneo maalumu kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa Ebola ambapo wizara ya Afya watayatangaza hivi karibuni.

Pamoja na mikakati hiyo waziri Aboud amewaomba waandishi wa habari kusaidia katika kusambaza elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa huo.

Akitaja dalili za ugonjwa huo Waziri Aboud amesema kuwa dalili kuu ni homa, maumivu makali ya kichwa, misuli na viungo vya mikono na miguu pamoja na koo.

Dalili nyengine ni kukosa nguvu za kiwiliwili na kufuatiwa na vipele katika ngozi,macho kuwa mekundu na kutokwa na damu katika tundu mbalimbali za mwili ikiwemo pua ,masikio mdomo na ngozi.

Kwa upande mwengine waziri ametaja njia zinazotumika kusambaza ugonjwa huo kuwa ni kugusana mojakwa moja na mtu aliyeambukizwa ,kugusa majimaji yanayotokana na mgonjwa kama vile damu,jasho, mate ,mkojo na makohozipamoja na kutumia vifaa vilivyotumiwa na mgonjwa mwenye maambukizi bila kusafisha vizuri.




Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>