Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Walimu waonywa kutotoza fedha wazazi

$
0
0
Na Kija Elias, Moshi
HALMASHAURI ya wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, imetoa onyo kali kwa walimu wakuu wa skuli za msingi wilayani humo, ambao wamekuwa na tabia ya kuwatoza fedha wazazi pindi wanapofuatilia cheti cha kuhitimu darasa la saba watoto wao.

Agizo hilolimetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Moris Makoi, wakati alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo, ambapo alisema wapo baadhi ya wazazi wamekuwa wakitozwa kiasi cha shilingi 10,000, na walimu wakuu wa skuli za msingi ili waweze kuwapatia vyeti hivyo.

Mwenyekiti huyo wa halmashauri, alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Fulgence  Mponji, kuwaandikia barua za onyo kali kwa walimu ambao wamekuwa na tabia za kuwatoza wazazi fedha ili waweze kuwapatia vyeti hivyo.

“Yapo malalamiko ya wazazi kutozwa fedha na walimu wakuu wa skuli za msingi katika wilaya yetu, na malalamiko haya yamenifikia ofisini kwangu, na baraza hili linakuagiza kuwaandikia barua za onyo walimu wanaowatoza fedha wazazi wanaofuatailia cheti cha kumaliza darasa la saba, kwani kwa kufanya hivyo wanaichafulia sifa halmashauri yetu,”alisema Makoi.

Alisema kitendo cha walimu wakuwatoza kiasi hicho cha fedha kwa lengo la kuwapatia cheti hakipo katika halmashauri yetu, na kwamba vyeti hivyo hutolewa bure na serikali hivyo mzazi anapofuatilia cheti cha mtoto wake ni vyema akapewa bure na si vinginevyo.


Kwa upande wao baadhi ya Madiwani ambao walipata fursa ya kuchangia maoni walihoji uhalali wa mzazi kutozwa fedha ndipo apatiwe cheti cha mototo wake, ambapo pia walitaka kujua fedha ambazo wamekuwa wakizitoa zinapelekwa wapi hata wanapodai risiti hawapewi.

“Kuna mchezo mchafu ambao unafanywa na walimu wakuu kwenye shule za msingi, mzazi anapokwenda shuleni kwa ajili ya kupata cheti cha motto wake aliyemaliza darasa la saba anatozwa fedha tena shilingi 10,000, ambayo haina maelezo yeyote yale,” walisema Madiwani hao.

Akijibu malalamiko hayo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, alisema kuwa hakuna uhalali wa kutozwa na kwamba maelekezo ya wizara ni kwamba cheti hicho hutolewa bure na hakilipiwi kamaambavyo wanafanya walimu hao.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>