Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Vigogo wengine kujiunga na ACT

$
0
0
Na Kadama Malunde,Shinyanga
 
CHAMA cha Alliance for Change and Transparency (ACT), kimewataka Watanzania kuacha kutumiwa na wanasiasa kama daraja la kufikia mafanikio.
 
Kimesema baadhi ya viongozi wa siasa wanawatumia Watanzania kujinemesha,huku wao wakiendelea  kubakia katika dimbwi la umasikini.
 
Aidha kimesema muda umefika wa kuleta mabadiliko na kuweka wazi kuwa ACT hakina mpango wa kuunga mkono CCM.
 
Akizungumza na wananchi wa manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya mahakama ya mwanzo Nguzo nane mjini,Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Kadawi Limbu,aliwataka wananchi kuwapuuza wanaosema wao ni CCM B.
 
Limbu alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwa makini na wanasiasa na kuchambua kwa kina kauli zao wanazozitoa majukwaani,kwani wengi wao wanatafuta njia ya kujineemesha na hawana uzalendo na nchi yao.

“Ndugu zangu, ACT siyo CCM B na wala hatuna mpango wa kuunga mkono CCM, hiki ni chama kipya kimeletwa kuwakomboa Watanzania,”alisema.
 
Naye Katibu wa vijana ACT Taifa, Philip Malack, alisema wanataka kuwaunga mkono Watanzania wanaopigania haki na kuomba  kuwapa ushirikiano, ili kufichua maovu yaliyojificha.
 
Alisema wapo vigogo kutoka vyama vingine vya siasa watakaojiunga na ACT hivi karibuni.
 
Alisema huo ni uzinduzi wa mkutano wa kwanza wa ACT kanda ya ziwa na kubainisha kuwa wataendelea kutembelea mikoa yote ili kufikisha ujumbe kwa Watanzania na kujitambulisha,huku akivitaka vyama vya upinzani kuacha kupotosha wananchi juu ya chama hicho.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ACT mkoa wa Shinyanga, Justina Kimisha, alisema chama hicho kimeweka mikakati ya kuleta mabadiliko tofauti na vyama vingine.
Aliwaomba wananchi kushiriki kikamilifu kwenye mikutano ili waone tofauti iliyopo na vyama vingine.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>