Na Magreth Kinabo, Dodoma
CHAMA cha Wakulima wadogo wa pamba Tanzania (TACOGA), kimemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, kusitisha mchakato wa bunge maalum la katiba.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu chama hicho, George Mpanduji, wakati akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba, Samuel Sitta,ofisini mjini Dodoma.
Mpanduji alieambatana na baadhi wa viongozi na wajumbe kutoka mikoa 11 wa TACOGA ,alisema wanaheshimu makubaliano ya kisiasa ya kutungwa katiba,lakini wana hofu kwamba katiba hiyo haitapatikana.
Aidha alishauri agenda za haki za jamii zipewe kipaumbele kwa kuwa kuna vilio vya kuhitajika suluhu za haraka baina ya jamii moja na nyengine.
Alisema wakulima wanataka katiba ipatikane haraka kwani itakuwa suluhisho dhidi ya mizozo na wafugaji, lakini wana hofu kwama azma hiyo inaweza kushindikana.
Kwa upande wake Sitta alisema lengo la bunge hilo ni kutunga katiba iliyo rafiki yenye kukidhi matakwa ya wananchi.