Na Mwandishi wetu
VIJANA wawili wameuawa kinyama baada ya kuchomwa moto wakiwa hai katika eneo la Tabata Liwiti wakituhumiwa kuiba pochi la mwanamke.
Walioshuhudia tukio hilo walisema,limetokea mwishoni mwa wiki ambapo baada ya kukwapua pochi hilo walikimbia na kuanza kufukuzwa.
Walipokamwa walipigwa vibaya na kisha kuchomwa moto hadi kufa.
"Matukio ya waendesha piki piki kukwapua yamekuwa yakitokea mara hapa Tabata na wanapokamatwa na wanapigwa na baadae kuchomwa moto kwa sababu wanapopelekwa vituo vya polisi wanaachiwa,” alisema mwanamke mmoja.