Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

DC mpya Chake Chake akabidhiwa mikoba

$
0
0
Na Maryam Salum,Pemba
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid  Abdalla, amewataka viongozi wa taasisi zilizo chini ya ofisi yake,kutoa ushirikiano wa hali ya juu, ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Alisema hayo  wakati akizungumza na wananchi, wafanyakazi, masheha,pamoja na viongozi wengine walio hudhuria katika hafla ya  kumkabidhi majukumu ya uongozi Mkuu mpya wa wilaya Chake Chake, Hanuna Ibrahim Massoud,kufuatia mabadiliko yaliofanywa na Rais wa Zanzibar hivi karibuni.

Alisema bila ya kuwepo ushirikiano kati ya wananchi na viongozi, mafanikio katika kazi zao hayatafikiwa.

Alisema iwapo wananchi watakuwa karibu na viongozi na kutoa ushirikiano wa dhati kwa viongozi, wilaya hiyo itapata mafanikio makubwa.

Alisema mkoa wa kusini umepata bahati kubwa ambapo mwanamke ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa kitendo ambacho hakijawahi kufanywa kisiwani humo.


Alimtaka Mkuu wa wilaya mpya   kuwashirikisha wananchi yakiwemo makundi mbali mbali katika kazi muhimu kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya na shehia.

Kwa upande wake mkuu mpya wa wilaya ya Chake Chake, Hanuna Ibrahim Massoud, alihimiza ushirikiano kutoka kwa wasaidizi wake ili wilaya hiyo iendelee kupata maendeleo.


Mohammed Juma Khatib, Mwenyekiti wa CUF Chake Chake, aliwataka Viongozi hao kumuhakikishia Rais kuwa wanawake wanaweza kwa kufanya kazi nzuri bila ya kusimamiwa na wanaume.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>