Na Haji Nassor, Pemba
Vijana kisiwani Pemba, wametakiwa kujiepusha na makundi ya watu wanaopita na kuwakusanya wakidai wanajadili rasimu ya pili ya katiba.
Kuali hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Zanzzibar (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka, wakati akizunguma na vijana wa chama hicho kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Gombani kongwe.
Alisema baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba, wamekuwa wakipita mitaani na kuwakusanya wananchi na kuichambua katiba hiyo,ambapo maoni yao hayapelekwi popote.
Alisema kwa vile vijana ndio nguzo ya kutegemea katika taifa, ni vyema wasighilibiwe kwa njia yoyote ile.
Alisema kwa sasa kazi ya kuichambua katiba hiyo inakwenda vyema na hakuna matusi tena kama ilivyokuwa awali.
Aliwahimiza vijana wa CCM kisiwani Pemba, kujipanga vyema na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ili kuhakikisha CCM inanyakua majimbo kisiwani humo.
Aidha alisema katika kufanikisha hilo umoja, mshikamano na utayari wa kila kiongozi na mwanachama unahitajika kwa nguvua zote.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa kusni Pemba, Abdalla Hamad Mshindo, aliwataka wanachama wa UVCCM kutembelea kifua mbele bila ya woga na kueleza ukweli juu ya kazi za CCM zinavyofanywa.
Katika risala yao, vijana wa mikoa miwili ya Pemba, walisema hatua ya Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shien, kuendelea kuisimamia vyema ilani ya CCM ni jambo la kuungwa mkono.