WAFANYABIASHARA wakubwa katika soko la Qatar lilipo mjini Chake chake Kisiwani Pemba, wameilalamikia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kuwatoza ushuru mara mbili, kwa bidhaa moja wanayosafirisha ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, huko katika soko hilo wafanyabiashara hao walisema kuwa wanatozwa ushuru mara mbili wakati wakisafirisha bidhaa zao.
Walisema kuwa wanapofika katika Bandari ya Tanga hulazimika kutozwa ushuru na TRA na baada ya kufika katika bandari ya Pemba hulazimika kutoa ushuru mara ya pili.
Mmoja kati ya wafanyabiashara hao Kassim Kishuka, alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawatoza ushuru mara mbili hali ambayo inawawia vigumu katika kufanya biashara zao.
“Kusema kweli Mamlaka ya MapatoTanzania inatuumiza katika suala zima la uchukuwaji na usafirishaji wabiashara zetu kwani wanavyotufanyia sisi wafanyabiashara sihaki”,alisema kwahuzuni .
Alielezakuwa hali hiyo inawasikitisha sana , maana wao wanafanya biashara kwa ya kujikwamua na halingumu ya maisha lakini wanachokipata ni cha maramoja na hakiwezi kuwa kukidhi katika mahitajiyao kutokana na ushuru huo.
Alifahamisha kuwa licha ya kutofikia malengo waliyojiwekea lakini pia kutokana nahali hiyo , yakutozwa ushuru marambili huwapelekea na wao kupandisha bei bidhaa zao.
Kwaupandewake mfanyabiashara, Juma Hussein, alisema kutokana na ushuru wa marambili kupitia TRA,unawafanya wafanyabiashara wengi kutofikia malengo yao waliyojiwekea.
Wafanyabiashara hao wakati wakilalamikia juu ya suala la kutoza kodi mara mbili na TRA, wameshindwa kuonesha risiti zinazo onyesha malipo ya ushuru wa marambili kutoka kwa mamlaka hiyo walipotakiwa kufanya hivyo na mwandishi wa habari hii.
‘’Ujua zile risiti nilikuwa nimeziweka hapa, lakini mbona sizioni au yule mwenzangu kaziondosha’’,alieleza mfanyabiashara huyo alipotakiwa kwa siku nne na mwandishi wa habari hizi kuonesha risiti hizo.
Akizungumzi hili Msaidizi Afisa Mdhamini Idara ya Forodha Pemba kutoka TRA Pemba, Abdalla Hassan Ali, alisema kuwa hakuna ushuru wowote, wafanyabiashara wanaotozwa mara mbili na TRA kama wanavyodai.
Alifahamisha kuwa, Bidhaa zinazotoka Tanzania bara, kuingia Kisiwani Pemba, hazitozwi Kodi ya yoyote na TRA, isipokuwa wafanyabiashara watakapokuwa hawana ‘Ankara ’ ya malipo yaushuru na ongezeko la thamani (VAT) yamzigo, hulazimika kutozwa asilimia mbili (2%) ya thamani ya bidhaa.
“Hii asilimia mbili tunazowatoza hawa wafanyabiashara ni ushuru waWizara ya biashara (Trade levy) lakini tunapokea sisi tukiwa kama ni mawakala wa Wizara hiyo, lakini haziingii TRA’’,alifafanua Afisa huyo.
Aliendelea kufafanua kuwa, Idara ya forodha inahusika zaidi na biashara za kimataifa, pamoja na kudhibiti uingiaji na utokaji wa vyombo vyote vya angani, baharini, pamoja na nchi kavu vinavyotoka nje ya nchi.
Alifahamisha kuwa, kodi inayolipwa na wafanyabiashara sio mara mbili, kwani kodi inayolipa na mfanyabiashara Pemba na anayolipa Mfanyadiashara waTanzania bara ni ileile ila mfanyabishara wa Tanzania bara analipa kwa taasisi moja na mfanyabiashara wa Pemba.
Pamoja na hayo msaidizi Afisa Mdhamini huyo,aliwataka wafanyabiashara wa soko hilo kufuata utaratibu wa ulipaji kodi kwa wakati kwa ajili ya maslahi ya nchi