Na Mwandishi wetu
KATIBU wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, amekumbwa na fyagio katika uhamisho wa Makatibu wa Mikoa uliofanywa na chama hicho.
Chatanda ambae alituhumiwa na Umoja wa Vijana wa CCM wa mkoa wa Arusha kwa kuingilia mambo ya ndani ya jumuiya hiyo, amehamishiwa mkoa wa Singida.
Zainab Shomari Katibu wa CCM mkoa wa kusini Unguja, anakwenda likizo kwa miezi miwili na Shija Othman Shija, amepelekwa mkoa wa Tanga kutoka kusini Pemba.
Mwangi Kundya, aliyekuwa Katibu wa mkoa wa mjini Unguja amehamishiwa Mbeya, Joyce Masunga amehamishiwa Pwani kutoka Mwanza, Alphonce Kinamhala amehamishiwa Arusha kutoka Katavi na Jeneth Kayanda sasa anakuwa Katibu wa mkoa wa Tabora kutoka Bukoba mjini.
Wengine waliohamishwa ni Gustav Muba anaekwenda Geita kutoka Tanga, Sauda Mpambalyota anaekwenda Kusini Unguja kutoka Pwani na Evelyne Mushi anaekwenda Katavi kutoka Kagera.
Aidha aliekuwa Katibu wa mkoa wa Singida, Naomi Kapambala, amehamishiwa Kigoma, Idd Ame amehamishwa kutoka Tabora kwenda Kagera, Mohamed Nyawenga amehamishiwa mjini Unguja kutoka Kigoma na Adam Ngalawa amehamishiwa Mara kutoka Shinyanga.
Maganga Sengelema amehamishiwa Shinyanga kutoka Mbeya, Marry Maziku, amehamishiwa makao makuu Dodoma kutoka Geita na Benard Nduta amehamishiwa Mwanza kutoka makao makuu Dodoma.
Wakara wa uhamisho huo ulisainiwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana.