Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Waziri Ferej azipongeza NGO’s

$
0
0
Na Khamis Haji, OMKR
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Fatma Abdulhabib Ferej, amesema serikali inathamini mchango unaotolewa na jumuiya za kiraia pamoja na vyombo vya habari katika kuielimisha jamii athari za mabadiliko ya tabianchi na kukabiliana nazo.

Aliyasema hayo jana alipofanya mazungumzo na ujumbe kutoka Jumuiya ya Zanzibar Climate Change Alliance ulioambatana na waandishi wa habari kutoka kituo cha TV cha East Africa Televisheni (EATV) ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar.

Alisema kutokana na uhalisia wake, Zanzibar ni eneo la visiwa hali inayosababisha kukumbwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo maji ya bahari kupanda juu na kula sehemu za ardhi inayotumika kwa kilimo na shughuli nyengine za kimaendeleo na kijamii.


Alieleza kuwa jukumu kubwa la taasisi hizo pamoja na vyombo vya habari ni kuandaa vipindi ambavyo vitatoa taaluma kwa wananchi kuweza kujiepusha na vitendo vinavyochangia athari hizo, ili Zanzibar ibaki salama.

Aidha, ujumbe huo ulimweleza Waziri Fereji kuwa wakiwa Zanzibar tayari wametembelea maeneo mbali mbali, ikiwemo kisiwani Pemba kwa ajili ya kujionea athari za mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kufanya mahojiano na wananchi wa maeneo tafauti juu ya chanzo na matokeo ya athari hizo.

Walisema lengo lao ni kuandaa vipindi vitakavyo tolewa kwa watazamaji, ili wananchi waweze kuwa na uelewa mpana zaidi juu ya mabadiliko ya tabianchi, athari zake na njia muafaka za kuweza kuchukua kujilinda.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>