Baadhi ya Wageni kutoka nchi tofauti wakipata huduma kutoka Uhamiaji mara baada ya kuwasili Uwanja wa Abeid Aman Karume. Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar.
Waziri Mbarouk amesema suala la Mashirikiano kwa wageni ni jambo muhimu linaloweza kuijengea sifa kubwa Zanzibar kwa wageni ambao wanakuja ambao wataweza kusimulia watakaoporudi ziara zao.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk Mwenye Koti Jeupe akipewa Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa uwanja wa ndege Juma Saleh.Katika ziara hiyo Waziri Mbarouk alitembelea maeneo tofauti ya Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume.
Maryam Himid/Saada Saleh-ZJMMC
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk amezitaka Taasisi zinazosimamia kupokea Watalii Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Amani Abeid Karume kujenga mashirikiano ili kuondosha usumbufu kwa wageni wanaoingia na kuotoka nchini.
Ameyasema hayo alipofanya ziara Uwanjani hapo kwa lengo la kuangalia hali halisi ya Wageni wanaoingia na kutoka nchini.
Waziri Mbarouk amesema suala la Mashirikiano kwa wageni ni jambo muhimu linaloweza kuijengea sifa kubwa Zanzibar kwa wageni ambao wanakuja ambao wataweza kusimulia watakaoporudi ziara zao.
Ametoa wito kwa Taasisi husika kuhakikisha Wageni wanaoingia Zanzibar wanapata huduma stahiki na ili kuepukana na usumbufu wa aina yoyote wanapofika katika Uwanja huo wa Ndege.
Amezitaja Nchi hizo kuwa ni pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Liberia na Siera leone ambapo amesema kila abiria kutoka nchi hizo lazima Apimwe ili kuweka kinga ya Ugonjwa wa Ebola nchini.
Hata hivyo Mkurugenzi wa uwanja wa ndege Juma Saleh Juma ameelezea baadhi ya changamoto zinazowakabili uwanjani hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa maeneo ya kukaribisha wageni,maegesho ya Magari na Uhaba wa Wafanyakazi wanaozungumza Lunga ya Kitaliano kutokana na Wataliano hao kutumia lugha yao tu.
Katika ziara hiyo Waziri Mbarouk alitembelea maeneo mbali mbali Uwanjani hapo ikiwemo Mapokezi, Maegesho ya Ndege na Magari na sehemu ya Mapumziko ya Abiria.