Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Zantel yadhamini semina za Fursa

$
0
0
 
Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, leo imetangaza kudhamini semina za kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa zilizopo nchini zitazoendeshwa kwenye zaidi ya mikoa 13 kwa kushirikiana na Clouds Media Group.
Semina hizo ambazo zinaenda sambamba na ziara ya kimuziki ya tamasha la Fiesta ambalo mwaka huu litaenda zaidi ya mikoa 13, zinatarajiwa kufanyika siku moja kabla ya tamasha kila mkoa ambao Fiesta inaenda.
 
Mada zitakazojadiliwa kwenye semina hizo ni pamoja na ubunifu, ujasiriamali, Uongezaji thamani kwenye bidhaa au shughuli yoyote unayofanya pamoja na kujenga ushirikiano, uwekezaji pamoja na lugha.
 
Akizungumzia semina hizo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, amesema kampuni yake imekuwa msitari wa mbele katika kuwawezesha vijana, na kwa semina hizi wanaamini vijana wengi watapata nafasi ya kuzitambua na kujifunza.
 
‘Tanzania ina fursa nyingi sana kwa vijana, na sisi Zantel tunaamini nafasi hii itakuwa muhimu kwa vijana kujifunza na kutambua fursa zilizopo kutoka kwa wataalamu mbalimbali’ alisema Khan.
 
Naye Mkurugenzi wa Utafiti na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alisema nchi ya Tanzania ina fursa nyingi lakini tatizo limekuwa ni namna ya kuzitumia fursa hizo.
 
‘Tumeandaa semina hizi kwa kutambua tatizo kubwa lilipo kwenye jamii yetu, umaskini na ukosefu wa ajira kwa vijana, jambo ambalo semina hizi zitaenda kutatua’ alisema Mutahaba.
 
Mojawapo wa wazungumzaji kwenye semina hizo atakuwa Mrisho Mpoto, mwakilishi wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF), Ruge Mutahaba pamoja na wageni waalikwa mbalimbali.
 
Kwa mwaka huu semina hizo zimeanzia mkoa wa Kigoma, katika Ukumbi wa Kibo Hall Park, na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya.
 

 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>